0


BALI, INDONESIA
BEKI wa Manchester United na timu ya taifa ya England, Chris Smallin amekimbizwa hospitali na baada ya kuumia vibaya akiwa katika mchezo wa kuteleza na barafu, Bali Indonesia.
Habari zinasema beki huyo ameumia usoni alipoanguka huku chanzo kikidaiwa ni kutokana na kula kichafu.
Picha zilimuonyesha beki huyo mwenye umri wa miaka 26 akiwa ameumia na akiwa na jeraha lenye ukubwa wa nchi tatu juu ya jicho lake la kulia huku mkono wake wa kushoto na shingo yake vikiwa vimefungwa bandeji.

Smallin alionekana akisaini kitabu cha kumbukumbu ‘autograph’ na jezi ya Manchester United za mashabiki wa timu hiyo wakati akiwa chini ya uangalizi wa madaktari.   
Smalling aliruhusiwa baada ya madaktari katika Kisiwa hicho cha Indonesia kuridhika na afya yake, huku United ikithibitisha taarifa hizo kwa kusema kwamba beki huyo alianguka baada ya kula chakula kichafu.

Waraka uliotolewa na mtandao wa klabu hiyo ulisomeka hivi: “Manchester United inaweza kufafanua Chris Smalling alikula chakula kichafu akiwa mapumzikoni ndiyo sababu ya kuanguka Jumapili.

“Beki huyo alikimbizwa hospitali na sasa anaendelea vizuri.
“Smalling kwa sasa yuko mapumzikoni baada ya kuitumikia England katika mashindano ya Euro 2016 kabla ya kuripoti kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu mwezi huu.” 
Beki huyo wa kati alisafiri kwenda barani Asia baada ya England kutolewa katika mashindano ya Euro na Iceland baada ya kupewa mapumziko na kocha Jose Mourinho.

Post a Comment

 
Top