BARCELONA,
HISPANIA
USHTUKE
ndiyo sheria hiyo. Lionel Messi amehukumiwa kifungo cha miezi 21 jela kutokana
na kukutwa na hatia ya kukwepa kulipa kodi.
Mamlaka
za kodi za Hispania zimemfikisha mahakamani Messi pamoja na baba yake, Jorge
Messi wakihusika katika kitendo cha
kukwepa kulipa kodi kati ya mwaka 2007 na 2009.
Baba
wa supastaa huyo wa Barcelona, Jorge naye amehukumiwa kifungo cha jela kutokana
na kukwepa kulipa kodi kiasi cha Pauni 3.5 milioni kwa kipindi cha miaka
miwili.
Wawili
hao pia wamepigwa faini ya mamilioni kwa kutumia kampuni zao za huko Belize na
Uruguay ambazo zimekuwa hazilipi kodi kutokana na mapato yanayopatikana
kutokana na mauzo ya taswira za mwanasoka huyo bora wa dunia mara tano.
Hata
hivyo, Messi na baba yake wanaweza wasifungwe jela. Kwa mujibu wa sheria za
Hispania, hukumu ya kifungo cha chini ya miaka miwili, mtuhumiwa anaruhusiwa
kutumikia kifungo chake nje akiwa chini ya uangalizi.
Mwanasoka
huyo na baba yake walikutwa na hatia kwa makosa matatu ya kukwepa kodi Jumatano na mahakama moja huko Barcelona.
Wakati
akijibu mashtaka hayo, Messi alidai kwamba hakuwa akitambua kitu kilichokuwa
kikifanywa na uongozi wake kwenye masuala ya pesa na kusema alichokuwa
akikifanya ni kucheza soka.
Messi
amepigwa faini ya Pauni 1.7 milioni, wakati baba yake amepigwa fainali ya Pauni
1.5 milioni.
Wachezaji
wengine waliokumbana na kasheshe la masuala ya kukwepa kodi ni Neymar, Javier
Mascherano, Adriano na Xabi Alonso.
Post a Comment