SHANGHAI,
CHINA
KUNA
watu wanapenda sana uchokozi. Huko China kuna shabiki mmoja alimjaribu Jose
Mourinho alipotua huko na kikosi chake cha Manchester United.
Wakati
mashabiki kibao wakiwa wamepanga mstari kuwapokea mastaa wa kikosi cha Man
United pamoja na kocha wao mpya Mourinho ili pia wawasainie jezi zao, kuna
shabiki mmoja amemjaribu Mreno huyo kwa kumpelekea jezi ya Chelsea.
Sawa,
Mourinho hata hata mwaka mmoja tangu aachane na klabu hiyo ya Stamford Bridge,
lakini unajua alichokifanya? Alimchunia shabiki huyo aliyekuwa ameshika jezi ya
Chelsea ile ya zamani yenye udhamini wa Samsung kifuani kama hajamwona vile.
Mourinho hakuisaini jezi hiyo.
Badala
yake aliandelea kufanya hivyo kwa kuzisaini jezi za Man United na vitabu na
majarida mengine ya mashabiki hao walioenda nayo mashabiki kwa ajili ya kupata
saini za wakali kutoka kikosi hicho cha Old Trafford.
Hata
hivyo, Mourinho hakuonyesha sura ya hasira kutokana na jaribio la shabiki huyo
kuona kama bado ana mapenzi na klabu hiyo aliyowahi kuinoa katika nyakati mbili
tofauti na kufanikiwa kuipa mataji matatu ya Ligi Kuu England.
Kocha
huyo wa zamani wa FC Porto, Inter Milan na Real Madrid alionyesha kutabasamu tu
kabla ya kumtambuka shabiki huyo na kuendelea na mambo mengine ya kusaini jezi
za mashabiki wengine.
Man
United jana Ijumaa ilitarajiwa kumenyana na Borussia Dortmund katika moja ya
mechi za kirafiki kujiandaa na msimu mpya wakati Jumatatu itakipiga na mahasimu
wao Manchester City huko huko China.
Post a Comment