MANCHESTER,
ENGLAND
JOSE MOURINHO amelithibitisha benchi lake la ufundi ambalo
litakuwa sambamba kusimamia majukumu ya Manchester United uwanjani.
Katika jeshi hilo, Luteni wa kuaminiwa, Rui Faria amekuwa
kocha msaidizi wa Mashetani hao Wekundu.
Kwa mara ya kwanza Mourinho alikutana na Faria walipokuwa Barcelona
kabla ya kufanya kazi kama kocha wa viungo wa Mourinho alipokuwa akiifundisha
Uniao de Leiria ya Ureno na akamfuata mara zote mbili alizojiunga na Chelsea,
Inter Milan na Real Madrid.
Silvino
Louro, ambaye amekuwa na Mourinho kwa zaidi ya miaka 10 akiwa kama kocha wa
makipa, pia ametajwa kuwa ni mmoja kati ya makocha wanne watakaojiunga na Mreno huyo Old Trafford.
Ricardo Formosinho na Carlos Lalin – ambao pia wana uzoefu
wa kufanya kazi na Mreno huyo – na Emilio Alvarez wote wamethibitishwa kuwa
sehemu ya benchi la ufundi sambamba na mchambuzi, Giovanni Cerra.
United
imehakikisha Mourinho anawapata washauri wote anaowaamini baada ya kocha huyo wa zamani wa Chelsea kuviambia
vyombo vya habari katika mkutano wake wa kwanza kwamba kuondoka kwa Ryan Giggs haukuwa uamuzi wake.
Katika mkutano huo wa kwanza uwanjani Old Trafford Jumanne,
Mourinho alisisitiza ilikuwa ni vigumu winga huyo wa zamani wa United kuendelea
kukaa klabuni hapo.
HILI NDILO JESHI KAMILI
RUI FARIA
Ana umri wa miaka 41-amemfuatana na Mourinho katika klabu za Porto, Chelsea, Inter Milan na
Real Madrid baada ya kufanya kazi na Mreno mwenzake huyo kama kocha wa viungo
katika klabu ya Uniao de Leiria.
Alifungiwa mechi nne Aprili mwaka 2014 baada ya kumtukana mwamuzi, Mike
Dean.
SILVINO LOURO
Amefanya kazi na makipa wazoefu wakiwemo Petr Cech na Julio
Cesar lakini anatarajiwa kupewa jukumu la jumla la ufundishaji. Akiwa na umri
wa miaka 57 amefanya kazi na Mourinho tangu Porto, Chelsea, Inter Milan na Real
Madrid.
RICARDO FORMOSINHO
Jukumu lake kubwa ni kufanya skautingi Manchester United. Akiwa
na umri wa miaka 59 amefanya kazi na Mourinho alipokuwa Porto na amefanya kazi
hiyo katika klabu 21 alipokuwa akifanya kazi hizo peke yake.
CARLSO LALIN
Mtaalamu wa viungo. Lalin atakuwa na kazi nyingi katika wiki chake zijazo kwa kuwa jukumu lake
litakuwa ni kuhakikisha wachezaji ambao Mourinho amewarithi wanakuwa fiti na
kuweza kufanya vizuri katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu England dhidi ya Bournemouth.
Alikuwa na jukumu kama hilo alipokuwa Chelsea.
EMILIO ALVAREZ
Pamoja na kwamba Louro
atakuwa ni mmoja kati ya makocha wa
benchi la ufundi, ni Alvarez ambaye atakuwa na kazi ya kuwaangalia David de
Gea, Sergio Romero na wengine.
Post a Comment