0


LIVERPOOL, ENGLAND
BAADA ya kurudi Anfield na kutamba kwamba anataka kubeba tuzo ya Ballon d'or akiwa mahali hapo, straika wa Kitaliano, Mario Balotelli (pichani) ametajwa kwenye orodha ya wachezaji watakaoachana na Liverpool kwenye dirisha hili la usajili.
Kocha Jurgen Klopp ameripotiwa kwamba anataka kuwa na wachezaji watakaokuwa tayari kucheza kwa kujitolea kwa asilimia 100 na jambo hilo linaweza kuwagharimu pia Christian Benteka na Jordon Ibe.
Tayari kocha huyo Mjerumani ameshawaondoa kwenye kikosi chake Kolo Toure, Jordan Rossiter, Jerome Sinclair, Joao Carlos Teixeira na Jose Enrique na jambo hilo linaweza kuwakuta wachezaji hao ambao walitarajiwa kuwamo kwenye kikosi cha kwanza cha miamba hiyo.
Liverpool haipo kwenye michuano ya Ulaya kwa msimu ujao, hivyo kocha Klopp anataka kuwa na kundi bora kabisa ambalo litahakikisha timu hiyo inafanya vizuri na kurejea kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao kwa kumaliza nafasi nne za juu kwenye Ligi Kuu England.
Wachezaji wenye uhakika wa kubaki ni Sakho, Lovren, Flanagan, Clyne, Gomes, Lucas, Allen, Coutinho, Lallana, Firmino, Can, Milner, Sturridge, Origi na Ings.

Post a Comment

 
Top