NA ABEID POLO
MABINGWA wa Tanzania Yanga wamelazimishwa
sare ya bao 1-1 na Al Ahly ya Misri katika mchezo wa kwanza wa Mabingwa Afrika uliochezwa
Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Kutokana na matokeo hayo, Yanga
imejiweka katika mazingira magumu pindi itakapoenda kcuheza mchezo wa marudiano
Misri dhidi ya miamba hiyo ya Afrika.
Mashabiki wa Yanga
Yanga itatakiwa kupata ushindi katika
mchezo huo au hata kulazmisha sare ya mabao zaidi ya 1-1.
Al Ahly ilikuwa ya kwanza kupata bao
katika kipindi cha kwanza, lililofungwa na Amr Gamal na Yanga ilisawazisha kwa
bao la kujifunga la beki wa Al Ahly kufuatia mpira uliopigwa na Issoufou
Boubacar na kumbabatiza beki Ahmed Hegazzy.
Gamal alifunga kwa kichwa akimalizia mpira wa adhabu ya Ramadan Sobhi. Bao la Yanga
lilipatikana katika dakika ya ya 18.
Katika
mchezo huo, Al Ahly ilikuwa ikicheza pasi fupifupi na kutawala mchezo ikiwa ni
mbinu ya kujihami na Yanga ilifanya makosa kuiga mchezo huo.
Shabiki akitabili matokeo.
Katika kipindi cha pili, Al Ahly
iliingia kwa kasi na kulisakama lango la Yanga kwa mipira merefu ya kushtukiza
lakini hadi mwisho mchezo huo uliisha kwa sare.
Kama Yanga itatolewa katika mchezo
utaochezwa Misri Aprili 19, mwaka huu itashindwa kufuzu kwa hatua za makundi ya
Ligi ya Mabingwa Afrika.
Hata hivyo, itaangukia katika michuano
ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
Mashabiki wa Al Ahly
Kikosi cha Yanga kilikuwa hivi: Ally
Mustafa ‘Barthez’(Dida) ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Kevin Yondan, Vincent
Bossou, Thabani Kamusoko, Deus Kaseke, Salum Telela, Amissi Tambwe (Simon Msuva),
Donald Ngoma, Issoufou Boubakar (Godfrey Mwashiuya).
Post a Comment