0


NA PRIVA ABIUD
 SI unamjua Pele? Ulishawahi kuona video zake? Naamini umesikia mengi kumhusu. Wabrazili wanaamini kuwa Pele ndiye Mungu wa soka. Ukibahatika kuona video zake na ukisoma takwimu zake, basi naamini nawe utakubali.
Miaka zaidi ya 2,000 iliyopita Malaika wa Mungu kwa Jina Gabriel, alitumwa kwa mrembo mmoja aitwaye Maria (Mariam) kuwa atamzaa Kristo yaani Yesu.
 Huyu malaika nadhani nimemwona tena Brazil ila kwa sura nyingine. Ndio. Kule Brazil nimemwona tena Gabriel, kwa sasa yupo pale Palmeras. Achana na Gabriel Boschilia yule aliyetoka Sao Paolo kwa na kuelekea Monaco huyu anaitwa Gabriel Jesus.

Huyu bwana mdogo amezaliwa mwaka 1997, hivyo ana miaka 19. Shughuli yake utadhani amezaliwa 90. Akiwa na miaka 18 tayari ameshaichezea timu ya wakubwa michezo 42 na kufunga mabao tisa.
Yaani jiulize, mtoto wa miaka 19 tayari amecheza michezo 42 Ligi Kuu ya Brazil. Hatari sana hii. Sasa. Kwa taarifa yako, alipokuwa na miaka 16 alifunga mabao 54 kwenye michezo 48!

Wapi Rashford! Achana na hilo akiwa na miaka 17 alifunga mabao 37 kwenye michezo 22. Wakati wewe unataka kujenga hoja kuwa Ligi ya Brazil ni laini Ronaldo de Lima amesema hii ni lulu kwa Wabrazili. Mnamo mwaka 2015 alitajwa kuwa mchezaji bora chipukizi wa Ligi Kuu ya Brazil kabla ya kukiongoza kikosi cha U-20 cha Brazil kwenye michuano ya Kombe la Dunia New Zealand.

Wakati namzungumzia huyu fundi, akili yangu imenirudisha nyuma kwa Adryan Tavares. Huyu bwana mdogo naye alitisha sana Flamengo, kisha akaelekea Leeds United na baadaye Flamengo, niliona kama Ronaldo mpya, nikaamini atafanya kile alichoshindwa kukifanya Pato. Lakini kwa sasa yupo kapuni, wakat naendelea kumuwaza Adryan mara wametokea kina Baschilio, Lima, na Malcom.
Hawa watoto ni moto wa kifuu. Sijui watapotea kama kina Ganzo au vipi. Roho inaniuma napomuona Moura, huenda maamuzi ya Jesus yakawa kama ya Moura kutamani pesa kuliko maisha yake ya baadaye ya soka yake.

Arsene Wenger anamfukuzia huyu dogo, Massimiliano Allegri naye ameonesha nia. Arsenal inaona Theo Walcott, Joel Campbell na Alex Oxlade-Chamberlain wameshindwa kazi, kama Gabriel ataelekea kule basi atapata nafasi na hasa ukiangalia thamani yake, uwezo wake n.k. Huyu dogo ukimuangalia unaweza kudhani ni Ronaldinho amenyoa, anapiga watu kanzu kama hana akili nzuri, anafunga utadhani Hamis Kiiza oooh sorry uthadhani Cristiano Ronaldo. Naamini muda si mrefu Gabriel ataleta taarifa kutoka Mbinguni Brazil.  Brazil ni mbingu ya soka.

 Huyu dogo aliiongoza klabu yake kuing'anya Santos ubingwa, kwa takwimu zake alicheza takriban dakika 1,300 na kufunga mabao manane, huku akitoa pasi tatu za mabao. Amepata kadi tano za njano nadhani kamzidi hata Daley Blind, na kadi nyekundu moja.
Kwa mtazamo huyu ni mpambanaji sio sharobaro. Mwanzon huyu dogo aligomea mshahara Real 15,000 za Kibrazili anmbazo sawa na Dola 4,200 hadi ukapanda kufikia Real 30,000 sawa na Dola 8,400.

Ila anaonekana kama mkorofi fulani hivi, maana juzi tu wakati anacheza dhidi ya Rosario Central alipiga bao kwenye droo ya 3-3 ila alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuzibuana na Damian Musto. Kama namuona Fellipe Mello vile. Anyway maneno yangu na mtazamo wangu sio sheria, nimemuona kwenye video mbalimbali, hivyo chochote chaweza tokea.
Ukitaka kumuona nenda Youtube andika Gabriel Jesus basi utamuona.

Post a Comment

 
Top