MANCHESTER, ENGLAND
WAYNE ROONEY nyota yake bado inang’ara kwa kutajwa kuwa
straika wa bora wa England mbele ya Harry Kane, kocha wa Manchester United,
Louis van Gaal amesisitiza.
Mjadala kuhusu nani anapaswa kuiongoza England katikan safu
ya ushambuliaji katika kipute cha Euro 2016 umepamba moto wakati Rooney
alipokuwa nje kwa miezi miwili kutokana na majeraha ya goti.
Rooney na Van Gaal
Lakini baada ya kuthibitisha kwamba nahodha huyo wa Man United
ataanza kuitumikia timu yake katika kikosi cha chini ya miaka 21 dhidi ya
Middlesbrough uwanjani Old Trafford Jumatatu usiku, Van Gaal amependekeza straika
huyo mwenye rekodi ya upachikaji wa mabao katika timu ya taifa ya England
anapaswa kupewa nafasi yake na kocha wa kikosi hicho, Roy Hodgson.
Rooney
“Unapoangalia rekodi yake, unamuona ni straika bora,”
alisema Mdachi huyo, huku akimtaadharisha Kane katika mchezo wa Jumapili
uwanjani White Hart Lane kwa kusema kuwa, straika huyo wa Spurs ana rekodi
mbaya katika michezo minne aliyocheza dhidi ya Man United.
“Kane ni straika mzuri
lakini hajafunga dhidi yetu,” alisema Van Gaal. “Ninaposema hivyo
ninampa changamoto pia, binafsi simuoni kama yuko makini.
Man United mazoezini
“Siku zote inategemea viwango. Kawaida, Rooney ni straika mzuri
lakini mara ngapi Kane amefunga kwa
jumla? Hiyo ni kazi ya straika, hata Wayne pai.”
Kane ameifungia Spurs mabao 25 msimu huu, ukilinganisha na Rooney
aliyeipachikia Man Unkited mabao 14.
Lakini Van Gaal anaamini kurudi kwa Rooney kutaipaisha Man United
katika kuwania kumaliza katika nafasi ya nne na kubeba Kombe la FA.
Van Gaal
Pia, Mdachi huyo aliweka wazi kwamba Rooney mwenye umri wa
miaka 30 anaweza kucheza mchezo wa marudiano wa robo fainali Jumatano dhidi ya
West Ham pamoja na kwamba amefanya mazeoezi na kikosi chake mara mbili tu mpaka
sasa.
Post a Comment