0


LONDON, ENGLAND
ARSENE WENGER amesema anatakiwa kuzifanyia ukarabati akili za wachezaji wake baada ya timu hiyo kutoka sare ya bao  1-1dhidi ya Crystal Palace,Jumapili.
Arsenal ilikubali bao la usiku la kusawazisha uwanjani Emirates pamoja na kutawala mchezo huo kwa zaidi ya asilimia 70.
Arsenal imepoteza pointi nyingine kwa mara ya pili mfululizo kufuatia sare ya 3-3 dhidi ya West Ham Jumamosi wiki iliyopita, bado iko na tofauti ya pointi 13 nyuma ya vinara wa ligi hiyo Leicester zikiwa zimebakia mechi tano.
Kauli hiyo ya Wenger inamaanisha sasa wanaangalia kubaki kwenye nne bora kuliko kutegemea Leicester itaanguka. Arsenal inashika nafasi ya nne,  nyuma ya Manchester City kwa tofauti ya mabao.

Sanches
"Baada ya mchezo huu sina tena hamu ya kuwaza ndoto za kutwaa ubingwa. Niko zaidi kwenye hamu ya kutengeneza upya uharibifu wa akili na kujiandaa kwa ajili ya mchezo unaokuja," Wenger alisema kwenye mkutano wa waandishi wa habari.
"Ni zaidi ya jambo hilo na angalia nyuma yetu. Kwa sababu kila mmoja anacheza vizuri na kushinda michezo. Kwetu itakuwa ni kupambana hadi mwisho kuishia kwenye nne bora. Kama tutaweza kujituma,  tutafanya zaidi. Lakini acha tuache kuota na tuangalie mchezo unaofuata."
Haya ni motokea mengine ya kukatisha tamaa kwa Arsenal, ambayo imejijengea utamaduni wa kupoteza michezo ambayo inapaswa kushinda.
Alexis Sanchez aliifanya timu hiyo kuongoza kabla ya mapumziko, lakini Yannick Bolasie alisawazisha kwa shuti la mbali katika dakika ya 82.
Na ilikuwa wazi huzuni  kwa Wenger ambaye alipaswa kuelezea anguko lingine la timu yake.
"Nimekata tamaa. Ni siku nyingine ambayo nisingependa kufanya mkutano baada ya mchezo kwa sababu hakuna jambo zuri," alisema.

Yannick Bolasie akisawazisha
"Ninahisi tulimiliki mpira kwa zaidi ya asilimia 70 lakini hata hivyo hatukufanya vya kutosha. Tulikosa umakini katika mipira ya mwisho na vilevile mabadiliko ya kasi.
"Hatukucheza kwa uhuru na kufuata mtiririko. Na mwishowe tuliadhibiwa kwa shuti la mbali la Crystal Palace. Walicheza kwa nguvu na kujilinda vizuri, na wakatukuta siye tumepumzika.  Hiyo hadithi ya mchezo, hata kama inakatisha tamaa."
Matokeo mengine Ligi Kuu
Jumapili
Bournemouth 1 Liverpool 2
Leicester 2 West Ham 2
Welbeck
Jumamosi
Norwich 0 Sunderland 3
Everton 1 Southampton 1
Man United 1 Aston Villa 0
Newcastle 3 Swansea 0
West Brom 0 Watford 1
Chelsea 0 Man City 3.

Post a Comment

 
Top