MANCHESTER,
ENGLAND
BOSI wa
Manchester United, Louis van Gaal amekiri straika wake, Wayne Rooney alipandwa
na hasira baada ya kutolewa katika mchezo wake wa kwanza Old Trafford baada ya kupona
majeraha ya goti.
Rooney hakucheza
vizuri katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Aston Villa na mashabiki walikuwa
wakimpigia kelele kwa kumfananisha na Gabriel Agbonlahor wa Villa ambaye
amekuwa mzito. Nahodha huyo
wa United mara ya mwisho kucheza mchezo wa Ligi Kuu ilikuwa ni Februari 13
dhidi ya Sunderland, alianzisha mpira
ambao Marcus Rashford alifunga bao hilo katika dakika ya 32 ya kipindi cha pili
lakini alitolewa katika dakika ya 67 na nafasi yake kuchukuliwa na Jesse
Lingard.
Jesse Lingard akingia, Rooney akitoka
“Alinichukia
kwa sababu alikuwa anataka kucheza kwa dakika 90,” alisema Van Gaal. “Lakini
mliweza kuona alivyokuwa akipoteza mipira – hajacheza kwa muda mrefu na siku
tatu za mazoezi haziwezi kutosha.
...akiwajibika uwanjani.
“Alicheza
vizuri katika kipindi cha kwanza lakini hakufanya vizuri katika kipindi cha
pili. Si jambo la kushangaza kwa sababu mzuka wa Ligi Kuu uko juu sana na
hajarudi katika ubora wake. Lakini sijaumizwa na kitendo chake hicho, inaonesha
ana ari ya kucheza dakika 90.”
Rooney alianza
kwa kucheza juu na Rashford lakini alishuka chini wakati mchezo ulipokuwa
ukiendelea. Mpira wa faulo wa haraka aliompigia Antonio Valencia ulimkuta Rashford
aliyefunga akiwa nje ya yadi nane kutoka lango la adui.
“Lilikuwa
pia bao la Rooney nadhani ,” alisema Van Gaal.
Kutokana na
Rooney kuvaa jezi ya nyekundu na nyeupe ya United ni habari nzuri kwa kocha wa
England, Roy Hodgson ambaye amepanga kumchukua straika huyo mwenye umri wa
miaka 30 kwenye fainali za Euro 2016.
Post a Comment