0




BARCELONA, HIPSANIA
BARCELONA imepigwa katika mchezo wa Ligi ya La Liga mabao 2-1 lakini Lionel Messi amefunga bao lake la 500 tangu aanze kucheza soka baada ya kuifungia timu hiyo Jumapili.
Messi ni mfungaji bora wa muda wote katika timu yake ya Barcelona na Ligi ya La Liga, akiwa amefunga mabao 500 katika michezo 632 aliyocheza.
Straika huyo mpaka sasa ana mabao 450 katika michezo 525 aliyoitumikia Barcelona na mabao 50  katika michezo 107 akiitumikia timu yake yake ya taifa ya Argentina.


wakitafakari kipigo
Pamoja na kwamba hajafunga katika michezo minne iliyopita, Messi amekuwa katika ubora wake mwaka 2016 baada ya kufunga mabao 26 katika michezo 28.
Mpaka sasa Messi amefunga mabao 309 ya La Liga na kumfanya kuwa na furaha mbele ya mpinzani wake Cristiano Ronaldo (256), wakati akiwa karibu kuifikia rekodi ya mabao 56 ya Gabriel Batistuta kwa aliifungia Argentina bao lake la 50 dhidi ya Bolivia wiki iliyopita.


Post a Comment

 
Top