LONDON,
ENGLAND
WAYNE ROONEY
ameibuka kinara wa mwaka 2016 kwa vijana matajiri wanamichezo wa Uingereza.
Rooney
mwenye umri wa miaka 30 akiwa ni nahodha wa timu ya taifa ya England na Manchester
United amejikusanyia utajiri wa Pauni 82 milioni na kumfanya kuongoza kwa
vijana wenye umri wa miaka 30 au chini ya miaka hiyo akiwa amepanda kutoka
Pauni 10 milioni za mwaka jana.
Utajiri wa Rooney
umekuja baada ya kupatikana ripoti kwamba analipwa Pauni 300,000 kwa wiki
katika mkataba wake Man United, ambao unamfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika Ligi Kuu
England, na vilevile mikataba aliyoingia na Nike na Samsung.
Andy Murray
Ndugu wawili
‘wanatenisi’ Andy na Jamie Murray wanashika nafasi ya pili kwa kuvuna Pauni 58 milioni,
pamoja na kwamba Pauni 57 milioni ni mchango unaochangwa na bingwa wa pili
duniani, Andy.
Mchezaji gofu, Rory McIlroy
anafurahia kwa kuongeza kipato kutoka Pauni18 milioni kumwezesha kumiliki jumla
ya Pauni 56 milioni na kushika nafasi ya tatu.
Mharishi huyo
wa Kaskazini amepata tuzo yenye thamani inayokaribia Euro 10 milioni, lakini
pesa yake anaipata kupitia dili zake na Kampuni za Nike, Omega, Bose, Upper
Deck sports memorabilia and Electronic Arts na kumfanya kuwa na faida kubwa.
McIlroy
Staa wa Real
Madrid, Gareth Bale anashika nafasi ya nne na kumfanya kuwa mwanasoka wa pili
kushika nafasi ya juu.
Bale
anaingiza kati ya Pauni 15.6 milioni kwa mwaka Bernabeu ukijumlisha na mikataba
yake ya Adidas, Sony and Electronic Arts. Ana thamani ya Pauni 34 milioni – ukilinganisha
na Pauni 13 milioni za mwaka jana.
Bale (kulia)
Wachezaji wa
kigeni wanaokipiga katika Ligi Kuu England ambao wapo katika 10 bora ni Sergio Aguero (Pauni 33 milioni), David Silva
(Pauni 31milioni), Radamel Falcao (Pauni 29 milioni), Samir Nasri (Pauni 22 milioni)
na Eden Hazard (Pauni18 milioni).
Nasri
Winga wa
Chelsea, Hazard anashika nafasi ya 10 pamoja na bondia, Amir Khan, ingawaje Khan
anaweza kuongeza kipato chake atakapocheza pambano lake dhidi ya Canelo Alvarez
mwezi ujao.
Khan
Mwaka jana,
Lewis Hamilton alikuwa tajiri wa jumla wa wanamichezo wote wa Uingereza kwa
kuwa na utajiri wa jumla wa Pauni 88 milioni.
Post a Comment