0


MADRID, HISPANIA
KARIM BENZEMA naye anaweza kuikosa Manchester City katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya  Jumanne baada ya kutolewa nje katika mchezo wa La Liga dhidi ya Rayo Vallecano.
Benzema alitolewa katika dakika ya 42 uwanjani Estadio de Vallecas na nafasi yake ikachulikuliwa na Lucas Vazquez. Baada ya kuingia Vazquez aliifungia Real Madrid iliyotoka nyuma kwa kufungwa mabao 2-0  na kupata ushindi wa 3-2.
Mfaransa, Benzema alionekana kujigonga katika goti lake la kulia, na kuwapa mashaka mashabiki wa Madrid waliofikiria anaweza kuukosa mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya uwanjani Etihad wiki ijayo.

Benzema
Real bado inahangaika kutaka kupona kwa Cristiano Ronaldo ili aweze kucheza mchezo huo dhidi miamba hiyo ya Ligi Kuu.
Ronaldo hakupangwa katika mchezo dhidi ya Vallecano baada ya kusumbuliwa na misuli  katika ushindi wa mabao 3-0  dhidi ya Villarreal Jumatano iliyopita.




Post a Comment

 
Top