0


LIVERPOOL, ENGLAND
MICHAEL OWEN amechaguliwa kuwa balozi wa kwanza wa kimataifa wa Liverpool  lakini taarifa hiyo haijapokelewa vizuri na baadhi ya mashabiki wa Anfield.
Mashabiki hao wengi wao wanahoji uamuzi wake wa kujiunga na wapinzani wao wa jadi Manchester United mwaka 2009.
Jukumu hilo litamfanya nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa England kuwawakilisha mashabiki wa duniani kote, pia ataiwakilisha klabu katika shughuli mbalimbali zikiwemo za kibishara.

...akiitumikia Man United
Owen aliibukia katika mpango wa timu ya vijana ya Liverpool kabla ya kufunga mabao158 katika michezo 297 akiitumikia Liverpool kwa misimu saba.

...akiitumikia Liverpool
Straika huyo alikuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya mwaka 2001 kwa kufunga mabao muhimu dhidi ya Arsenal na kushinda Kombe la FA.
Hata hivyo, uamuzi wa Owen kuhamia Real Madrid mwaka 2004 na kujiunga na United – ambako hatimaye alishinda Kombe la Ligi Kuu 2011-  umekuwa mchungu katika midomo ya mashabiki wa Liverpool.

...ni pekee kwa Liver kushinda, Ballon d'Or mpaka sasa.
Wengi walitoa maoni yao kwenye mitandano ya kijamii baada ya Owen kutangazwa Alhamisi.
Baadhi ya maoni yalisema 'Mchezaji wa Man United, Michael Owen? Hapana, asanteni, 'Ni bora hata ya El Hadji Diouf' na 'Nyoka amekuwa balozi wetu wa kimataifa.' 


Post a Comment

 
Top