0


LONDON, ENGLAND
HARRY KANE (pichani juu) anayeongoza katika upachikaji wa mabao Ligi Kuu England ametajwa katika listi ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji wa kulipwa (PFA).
Mbali na Kane anayekipiga Tottenham, fundi wa mpira, Mesut Ozil wa Arsenal naye ametajwa sambamba na kiungo wa West Ham, Dimitri Payet.

Vardy
Listi hiyo ya wachezaji sita inawajumuisha wachezaji watatu wa kocha wa Leicester City, Claudio Ranier ambaye kikosi chake kipo mbioni kutwaa taji la Ligi Kuu, Jamie Vardy, Riyad Mahrez na N'Golo Kante.
Hilo limewafanya mashabiki wa Manchester United kununa baada ya straika wao kinda, Anthony Martial kutokuwamo kwenye listi hiyo.

Martial
Mfaransa huyo ambaye ameuanza vizuri msimu wake wa kwanza katika Ligi Kuu, kitu ambacho kinawapa kiburi mashabiki wa United kupandwa na hasira.
Mahrez anahofiwa kutwaa tuzo hiyo kutokana na kuwa na msimu mzuri Leicester.
Muargeria huyo ameifungia Leicester mabao 16 na ametoa asisti 11.
Vardy naye anapewa nafasi kutokana na kuvunja rekodi ya upachikaji mabao. Staa huyo alivunja rekodi ya Ruud van Nistelrooy ya kufunga katika kichezo 11 mfululizo.
Vardy (29) amefunga mabao 21 katika Ligi Kuu akimfukuzia straika mwenzake wa timu ya taifa ya England, Harry Kane ambaye pia ameingizwa kuwania tuzo ya Mchezaji Kijana.
Straika huyo wa kikosi kinachonolewa na Mauricio Pochettino amepachika mabao 22 katika Ligi Kuu na kuisaida Tottenham kushika nafasi ya pili.

Ozil
Ozil ameingia katika listi hiyo baada ya kuisaidia Arsenal kwa kutoa asisti 18 wakati Payet ameanza vizuri msimu wake wa kwanza Upton Park.
Katika kuwania mchezaji kijana wa mwaka wa PFA, Kane anaungana na nyota mwenzake wa Spurs, Dele Alli na wachezaji wa Everton, Romelu Lukaku na Ross Barkley na kipa wa Stoke City, Jack Butland na kiungo wa Liverpool, Philippe Coutinho.
Wanaowania PFA
N'Golo Kante, Riyad Mahrez, Jamie Vardy (All Leicester), Mesut Ozil (Arsenal), Dimitri Payet (West Ham), Harry Kane (Tottenham)
Mchezaji kijana wa PFA
Dele Alli, Harry Kane (Both Tottenham), Ross Barkley, Romelu Lukaku (Both Everton), Jack Butland (Stoke), Philippe Coutinho (Liverpool)
Mchezaji wa PFA  wa mwanamke  Ji So-Yun, Hedvig Lindahl, Gemma Davison (All Chelsea), Izzy Christiansen (Manchester City), Beth Mead (Sunderland)
Mchezaji kijana wa  PFA mwanamke
Beth Mead (Sunderland), Nikita Parris, Keira Walsh (Manchester City), Hannah Blundell (Chelsea), Danielle Carter (Arsenal)

Post a Comment

 
Top