NYON,
SWITZERLAND
MANCHESTER CITY
itacheza dhidi ya Real Madrid katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Tofauti na utabiri wa
watu wengi kwamba Man City ingeweza kucheza na Buyern Munich inayofundishwa na kocha wake mtarajiwa, Pep
Guardiola.
Man City iliitoa Paris
Saint-Germain katika hatua ya robo fainali
kwa bao la Kiungo Mbelgiji, Kevin De Bruyne aliyeihakikishia ushindi
wa bao1-0 uwanjani Etihad na kuifanya
miamba hiyo Ligi Kuu England kupita kwa
jumla ya mabao 3-2.
Real Madrid ilifufuka
baada ya kichapo cha mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza dhidi ya Wolfsburg na
kusonga mbele kufuatia ‘hat-trick’ ya mchezaji wa zamani wa Manchester United, straika
Cristiano Ronaldo.
Ronaldo na nyota mwenzake
wa zamani wa Ligi Kuu, Gareth Bale watarudi England.
Man City itaanzia
nyumbani katika mchezo wa kwanza
utakaopigwa Aprili 26 au 27 kabla ya mchezo wa marudiano uwanjani Bernabeu
wiki moja baadaye.
Timu hiyo ya ‘Wananchi’
ilikutana na Real Madrid katika Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi msimu wa 2012-13.
Katika mchezo wa
kwanza uliopigwa Bernabeu, Real iliifunga City mabao 3-2 kwa mabao ya Marcelo, Karim Benzema na Ronaldo,
wakati mabao ya Man City yalifungwa na Edin Dzeko na Aleksandar Kolarov.
Kipa wa Man City, Joe Hart akishangilia na Fabiani Delph. Mchezo wa marudiano
jijini Manchester uliisha kwa sare ya bao 1-1, bao la penalti la Sergio Aguero likiwa
la kusawazisha baada ya Benzema kuipa Real bao la kuongoza katika dakika ya 10.
Nusu fainali nyingine
itakuwa itazikutanisha Atletico Madrid, ambayo iliitoa Barcelona, dhidi ya Bayern
Munich, inayonolewa na Guardiola ambaye hizi zitakuwa fainali zake za mwisho
kabla ya kuanza majukumu mapya Man City msimu ujao.
Ronaldo atarudi jijini Manchester
Kuna historia
ilizozikutanisha Bayern Munich na Atletico Madrid zilipokutana mwaka 1974 katika
fainali ya Kombe la Ulaya.
Mchezo wa kwanza uliofanyika
Heysel Brussels uliisha kwa sare ya bao 1-1baada ya dakika 120, baadaye Bayern
ilishinda mabao 4-0 katika mchezo wa marudiano kwa mabao ya Gerd Muller na Uli
Hoeness.
Post a Comment