MANCHESTER, ENGLAND
YAYA TOURE anaondoka Manchester City mwishoni mwa msimu,
wakala wake Dimitri Seluk amethibitsiha
Kiungo huyo mkataba wake unafikia kikomo Juni na hivyo kuhitimisha
miaka sita ya kuitimikia klabu hiyo.
Seluk, amekuwa akifanya mazungumzo na maofisa wa Man City katika
wiki za hivi karibuni lakini wameamua kutafuta maslahi sehemu nyingine.
...akiwa na Kombe la FA.
“Ni dhahiri anaondoka Manchester City, bila shaka naweza
kuthibitisha hilo,” alisema.
“Ofa kadhaa zimewasili kwa ajili ya Yaya na tunazitathimini, lakini bado hatujafanya uamuzi wapi atakwenda msimu ujao.”
“Ofa kadhaa zimewasili kwa ajili ya Yaya na tunazitathimini, lakini bado hatujafanya uamuzi wapi atakwenda msimu ujao.”
Wasiwasi ulianza juu ya Toure kuendelea kuwapo Man City
baada ya kutangazwa kwamba kocha Pep Guardiola atachukua mikoba ya Manuel
Pellegrini mwishoni mwa msimu.
Guardiola alikuwa ni
kocha aliyemuuza Toure Manchester City akitokea Barcelona kwa Pauni 24 milioni. Toure alikuwa akijiandaa
kuchezaji chini ya bosi anayekuja, lakini sasa amechukua uamuzi wa kuondoka.
Toure atakuwa na furaha kujiunga na klabu nyingine ya Ligi
Kuu kama ataamua kuachana na kiasi kikubwa cha pesa kama atakwenda China au
Mashariki ya Kati.
Akiwa na umri wa miaka 32, bado anaweza kuwa na mchango
mkubwa katika klabu.
...sambamba na Kompany
“Kipengele cha kiuchumi kimeleta mabadiliko? Bila shaka hapana,”
Seluk alisema: “Hatukuweka pesa mbele ya kila kitu lakini mradi wa klabu unatutoa.
Kitu bora kitatushawishi.”
Aidha
inadaiwa Toure anaweza kurudi kwa kocha Roberto Mancini wa Inter Milan, ambaye
alimnunua Toure katika miaka yake mitatu ya kwanza kabla ya kufukuzwa Man City,
wazo hilo liko wazi kwa Toure.
Seluk: hakuna budi, Yaya anaondoka
Seluk aliongeza: “Inter? Bila shaka tunaizungumzia timu
kubwa na kila mmoja anajua uhusiano uliopo kati ya Yaya na Mancini, lakini kama
nilivyotangulia kusema, bado hatujafanya uamuzi.
“Lakini niongeze kwamba mradi wa ‘Nerazzurri’ ni mzuri na Inter
ni klabu nzuri. Pia , ni kawaida kumtaka mchezaji wa levo yake.”
Post a Comment