LONDON, ENGLAND
CHELSEA imemthibistisha Antonio Conte kuwa kocha mpya wa
timu hiyo msimu ujao pindi atakapomalioza
kuitumikia Italia katika mashindano ya Euro 2016 na ameshasaini mkataba
wa miaka mitatu.
Conte ambaye dili lake lina thamani ya Pauni 4.75 milioni kwa
mwaka baada ya kukatwa kodi, alisema: “Nina furaha isiyo kifani kupata heshima ya kuifundisha Chelsea. Ninajivunia
kuwa kocha wa timu yangu ya taifa na nitaendeleza jukumu langu kama hilo
nitakapoanza kazi Chelsea.
Conte
“Ninaangalia mbele kukutana na kila mmoja klabuni na siku baada ya siku
nitakutana na changamoto za Ligi Kuu England.
“Chelsea na soka la England zinaangaliwa kila unapokwenda, mashabiki
wana shauku na tamaa yangu ni kuwa na mafanikio zaidi kuendeleza ushindi
niliokuwa naufurahia nilipokuwa na Italia.
“Nimefurahi tumetangaza Leo na sasa kila kitu kitakuwa sawa
na tunaweza kumaliza tetesi. Nitaendelea na kibarua changu kama kocha wa timu
ya taifa ya Italia na sitaiongelea Chelsea hadi baada ya kumaliza kwa
mashindano ya Euro.”
Mkurugenzi wa Chelsea, Marina Granovskaia amesema klabu
inaangalia mbele katika msimu msimu ujao itakapokuwa chini ya uangalizi wa Conte.
“Tuna furaha kuwa na mmoja wa makocha anayeangaliwa sana
katika ulimwengu wa soka na tumefurahi kulitimiza hilo kabla ya msimu huu
haujafikia mwisho. Hii inasaidia katika mipango yetu ya baadaye,” Granovskaia
alisema.
Conte mwenye umri wa miaka 46
amekuwa kocha wa Italia tangu mwaka 2014,
kufuatia kujiuzulu kwa Cesare Prandelli baada ya Italia kutolewa katika Kombe la Dunia lililofanyika
Brazili sambamba na England katika Kundi D.
Chini yake Italia imefuzu katika fainali za Euro 2016 bila
ya kupoteza mchezo na itapamba na Ubelgiji, Ireland na Sweden katika hatua ya
makundi.
Conte
Kabla ya kupewa jukumu la kufundisha timu ya taifa ya Italia,
Conte aliiongoza Juventus kwa misimu mitatu na kushinda Ligi Kuu ya Italia Serie
kila mwaka.
Katika enzi zake za kusakata soka, Conte alikuwa kiungo
aliyecheza michezo 400 akiitumikia Juventus
kuanzia mwaka 1991 hadi 2004, akishinda Ligi ya Serie A mara tano.
Post a Comment