MANCHESTER,
ENGLAND
LOUIS
VAN GAAL hana mpango wa kuondoka Manchester United leo wala kesho, kwani ndio
kwanza anapanga mipango ya msimu ujao.
Mdachi
ambaye hatima yake ipo shakani ikidaiwa nafasi yake itachukuliwa na, Jose
Mourinho.
Van
Gaal amedokeza mipango yake ya msimu ujao ndani ya Man United na kutoa ishara
kwamba bado ataendelea kuwapo Trafford msimu ujao licha ya mashabiki wengi
kumlaumu kwa msimu mbovu klabuni hapo.
“Nipo
katika hatua ambayo inanihusisha kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao na ni
mimi ndiye ambaye nimeamua tutakwenda China kwa siku nane,” alisema Van Gaal
mwenye umri wa miaka 34.
...akifungua makabrasha mbele ya Giggs.
“Nimewahi
kwenda China hapo awali na pia nimewahi kucheza kama mchezaji pale Shanghai.
Hatukuweza kufanya mazoezi vizuri kwa sababu ya hewa nzito. Tunakwenda kwa
sababu za kibiashara tu. Nikiwa kama kocha wa Manchester United najua ni nini
tunapaswa kufanya,” aliongeza kocha huyo.
“Lakini
pia nimeweka wazi kwamba hatutakaa kwa zaidi ya siku nane. Baada ya hapo
tutarudi kwa ajili ya kufanya mazoezi. Hayo sio maandalizi mazuri na ni vigumu
kwa sababu itabidi tufkirie pia kuhusu mechi za Ligi ya mabingwa.”
...akitoa maelekezo kwa Rooney.
Kuonyesha
kuwa Van Gaal bado yupo yupo sana Manchester United kocha huyo pia amezungumzia
masuala ya usajili wa wachezaji kwa ajili ya msimu ujao huku akimgusia
mshambuliaji wa Everton, Romelu Lukaku ambaye amekuwa akihusishwa kwenda United
kwa dau kubwa.
...akifanya dhihaka
“(Lukaku)
anavutia sana. unapofunga mabao mengi lazima utakuwa unatakiwa na klabu kubwa.
Mchezo wa soka ndivyo ulivyo. Ukiangalia mabao aliyofunga na pasi za mabao
alizopiga, Lukaku anafanya hivyo katika kiwango cha juu Ligi Kuu ya England.
Nadhani kila klabu duniani inahitaji washambuliaji,” alisema Van Gaal.
Naye
Mwandishi mashuhuri wa Gazeti la Sunday People la Uingereza, Steve Bates alidai
kwamba kuna uwezekano mkubwa Van Gaal akabakia United kutokana na mipango
ambayo amekuwa akihusishwa kuifanya, huku akidai kwamba Bosi Mtendaji wa
United, Ed Woodward hataki kumfukuza kocha huyo.
“Nguvu
aliyonayo Van Gaal katika kuandaa safari hiyo inashtua sana hasa wakati ambapo
watu wengi tuliamini kuwa alikuwa anaishi kama mtu ambaye ameshakufa.
“Kwa
klabu kumruhusu awe katika nguvu hizo na jinsi walivyojipanga kwenda China
inaonyesha kuwa atabakia,” alisema Bates.
...dogo bado unaitaka nafasi yangu?
“Ed
Woodward hataki kumfukuza Louis van Gaal na mechi chache zijazo zitakuwa muhimu
kwa sababu kama United itaingia Top Four na itatwaa Kombe la FA sidhani kama
atafukuzwa,” aliongeza Bates.
Bates
amedokeza kwamba inadaiwa kuwa mabosi wa United walikuwa wanataka kucheza mechi
tatu hadi nne wakiwa China kwa ajili ya kujitangaza zaidi lakini Van Gaal
amefanikiwa kuwashawishi kucheza mechi mbili tu kitu ambacho kinaashiria kuwa
ana nguvu ndani ya klabu hiyo na huenda akabakizwa msimu ujao.
Post a Comment