LIVERPOOL, ENGLAND
LIVERPOOL imepambana
kufa na kupona dhidi ya Borussia
Dortmund usiku wa Alhamisi na kuibuka wababe na kufuzu kwa hatua ya
nusu fainali.
Timu hiyo ya Anfield ikicheza katika uwanja wake wa nyumbani
iliweza kufungwa bao la kwanza katika dakika tano ya mchezo lililopachikwa na kiungo, Henrikh Mkhitaryan.
Lovreeeen.....
Ilipotimia dakika ya tisa, Dortmund iliandika bao la pili
kupitia straika wa kimataifa wa Gabon,
Pierre-Emerick Aubameyang na wengi wakaamini kuwa ulikuwa ni mwisho wa Liverpool.
Hata hivyo, Liverpool iliweza kujitutumua kupitia bao la
kwanza lililofungwa Divock Origi dakika ya 48.
Baadhi ya mashabiki wa Liverpool walikata tamaa, baada ya
timu hiyo kupachikwa bao la tatu katika dakika ya 57 lililofungwa na kiungo mshambuliaji, Marco Reus.
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp.
Lakini dakika ya 66 mambo yalibadilika na Liverpool kupitia
kiungo wake Mbrazili, Philippe
Coutinho iliweza kupata bao la pili na kuyafanya matokeo kusomeka 2-3.
Dakika ya 77, ndipo Liverpool ilipoweza kuweka mambo sawa
nakusawazisha bao la tatu kupitia kwa beki wake Mamadou
Sakho.
Hapa ni shangwe na majonzi.
Ndipo ilipokuja dakika ya faraja, ile ya 91, beki Dejan Lovren
alipoihakikishia Liverpool kucheza nusu fainali ya Kombe la Europa League baada
ya kufunga bao la nne.
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Ujerumani zilitoka sare ya
bao 1-1 hivyo, Liverpool imepita kwa ushindi wa mabao 5-4. Kwa ushindi huo,
Majogoo hao wa Anfield watacheza na Wahispania, Villareal.
Aubameyang
Wakati huohuo, Wahispania
Villarreal ilishindi dhidi ya Sparta Prague, Sevilla iliifunga timu nyingine ya
Ligi ya La Liga, Athletic Bilbao, na Shakhtar Donetsk ilipiga kirahisi dhidi ya
Wareno, Brag.
Kama ilivyokuwa kwa
Dortmund, Kocha Jurgen Klopp atacheza mchezo wa marudiano Merseyside,
baada ya Liverpool kusafiri kwenda Estadio El Madrigal kwa ajili ya mchezo
wa kwanza - Hii ni mara ya kwanza kwa Liverpool
na Villarreal kukutana katika mashindano ya Ulaya.
Liverpool wapagawa.
Mchezo wa kwanza kati ya Shakhtar Donetsk dhidi ya Sevilla utapigwa
Ukraine na ule wa marudiano utachezwa Ramon Sanchez Pizjuan.
Mchezo wa kwanza wa nusu fainali utapigwa Aprili 28 na ule
wa marudiano utakuwa wiki moja baadaye Mei 5.
Mwaka huu fainali itachezwa
katika Uwanja wa St Jakob-Park jijini Basle, Switzerland Mei 18.
Post a Comment