MANCHESTER,
ENGLAND
SIR
ALEX FERGUSON amemuonya kocha mtarajiwa wa Manchester City, Pep Guardiola.
Ferguson
ambaye ni kocha wa zamani wa Manchester United, amemwambia Guardiola kwamba asitegemee
mteremko katika Ligi Kuu ya England kama alivyoupata akiwa na Barcelona ya
Hispania katika La Liga, au na Bayern Munich katika Bundesliga.
Babu
Ferguson ambaye kwa sasa ana miaka 74 anaamini kwamba Man City imeokota dhahabu
kwa kufanikiwa kumnasa Guardiola kutoka Bayern Munich, lakini anaamini kwamba
itakuwa vigumu kwa Mhispaniola huyo kurudia mafanikio yake akiwa Ligi Kuu ya
England na Man City.
“Itakuwa
vigumu sana kwake kurudi kile alichokifanya Barcelona. Ni wazi kwamba Man City
imelamba dume kumpata kwa sababu ni bonge la kocha lakini Pep hatapata njia rahisi
sana Ligi Kuu ya England,” alisema Ferguson.
“Soka
la Kiingereza sio rahisi. Kila kocha wa kigeni ambaye amekuja England
atakwambia hivyo. Arsene Wenger, baada ya miezi michache alikuwa anaongelea
jambo hilo hilo. Jose Mourinho baada ya msimu wake wa kwanza alitambua kwamba
angeweza kufanikiwa kwa kufanya kazi ngumu sana,” aliongeza Ferguson.
Guardiola
“Nadhani
Pep atapata mafanikio, lakini sidhani kama ataweza kurudia kile alichokifanya
Barcelona. Kile kilikuwa kiwango kikubwa. Walikuwa katika ubora wao.”
Ferguson
amepoteza mechi mbili za fainali kwa Guardiola. Fainali ya kwanza ilikuwa mwaka
2009 wakati walipochapwa mabao 2-0 dimba la Olimpiki katika Jiji la Rome kwa
mabao ya Samuel Eto’o na Lionel Messi.
Fainali
nyingine ni ya mwaka 2011 wakati walipochapwa mabao 3-1 dimba la Wembley ardhi
ya nyumbani England kwa mabao ya Pedro, David Villa na Lionel Messi huku la
United likifungwa na Wayne Rooney.
Ferguson na Guardiola
Pamoja
na vichapo hivyo, Ferguson anakiri kumkubali Guardiola kwa kazi nzuri
anayoifanya katika timu zake anazofundisha na amewaonya wachezaji legelege wa
Manchester City kuwa wasitarajie kufanya kazi nyepesi kwa Guardiola.
“Pep
bila shaka ana nidhamu kubwa ya kazi yake. Anahimiza sana hilo katika mazoezi
yake yote kwa hiyo yeyote ambaye anafikiria hatafanya kazi kubwa, basi hatadumu
muda mrefu kwake. Nina uhakika na hilo, ana uwezo mkubwa sana wa ukocha,” alisema
Ferguson.
Post a Comment