BARCELONA,
HISPANIA
LIONEL
MESSI na Cristiano Ronaldo wataingia katika vita nyingine kali ya mchezo wa ‘El
Clasico’ pale Barcelona itakapopambana na Real Madrid Jumamosi hii. Masupastaa hao- ambao wana upinzani binafsi katika historia ya soka - watazing’arisha klabu zao katika mchezo huo wenye upinzani mkubwa.
Huu utakuwa mchezo wa 25 uwanjani Nou Camp katika El Clasico kuwakutanisha Messi na Ronaldo tangu staa huyo Mreno alipoondoka Manchester United mwaka 2009.
Kila mmoja, Ronaldo na Messi kila mmoja ameisaidia timu yake kupata ushinda mara 12 na kuufanya mchezo huu wa Jumamosi kuwa muhimu zaidi.
Ronaldo
Lakini Messi na Barcelona wanapewa nafasi kubwa ya
kupata ushindi na kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa taji la La Liga. Ikiwa imebaki michezo sita, Barcelona iko mbele kwa pointi 10 dhidi ya Madrid- ambayo inashika nafasi ya tatu nyuma ya wapinzani wao wa Jiji la Madrid, Atletico Madrid.
Messi
Lakini kikosi hicho cha kocha Zinadine
Zidane kinaweza kupata ushindi wa ugenini- na kwa kushangaza Ronaldo mwenye
mabao 28 kwenye ligi ndiye anayeweza kufanikisha hilo.
Post a Comment