MANCHESTER, ENGLAND
MANCHESTER CITY imeongeza matumaini
ya kuinasa saini ya straika, Lionel Messi mwishoni mwa msimu baada ya
mazungumzo ya mkataba kati ya staa huyo wa Argentina na klabu yake ya Barcelona
kukwama. Na kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika mazungumzo kati ya pande hizo mbili yako mbali kufikia muafaka.
Man
City imewaambia wawakilishi wa Messi mwenye umri wa miaka 28, kwamba iko tayari
kumlipa Pauni 800,000 kwa wiki na kumuunganisha na bosi wake wa zamani Pep
Guardiola.
Messi anataka kuongezwa mkataba wa
miaka mitatu na Barcelona na mkataba wake wa sasa unaisha mwishoni mwa mwaka 2018.
Messi akifunga bao dhidi ya Bayern Munich.
Rais
wa Barcelona, Josep Bartomeu amemuonya baba wa mchezaji huyo na wakala
wake kwamba klabu hiyo haiwezi kumudu mahitaji ya mkataba huo unaotakiwa.
Man
City imeweka wazi kwa wawakilishi wa Messi kwamba wako tayari kutimiza lengo
lake kwa kumpa mkataba wa miaka mitano.
Barcelona
haitaki kumpa Messi miaka mitatu Messi kwa kuhofia staa huyo atawatia hasara mbele
ya safari kwa kuwa atakuwa anakula pesa
za bure baada ya kuisha kwa kipaji chake.
Post a Comment