LONDON, ENGLAND
DIEGO COSTA ameshawishika kubaki Stamford
Bridge baada ya kufanya mkutano wa siri na bosi mpya wa Chelsea, Antonio Conte.
Conte, ambaye atachukua nafasi ya kocha wa muda, Guus Hiddink mwishoni mwa msimu, amekutana na Costa Jumanne katika viwanja vya mazoezi vya klabu hiyo, Cobham alipoenda kukitembelea kikosi hicho kwa mara ya kwanza.
Na bosi huyo wa sasa wa timu ya taifa ya Italia amemshawishi Costa kuachana na mawazo ya kutaka kurudi Hispania msimu ujao.
Costa
Chanzo cha ndani ya klabu hiyo kimethibisha
kwamba Conte amemhakikishia Costa, 27, kwamba anamhitaji katika mpango wake wa
kuijenga upya Chelsea mpya, ingawaje straika huyo ametawaliwa na mawazo kwamba
hatendewi haki na waamuzi wa Ligi Kuu. Kumbakisha Costa ni kazi nzuri kwa Conte, ambaye anapambana kufanya kazi ya kuijenga upya klabu hiyo huku akipanga kuwaongeza baadhi ya mastraika wengine.
Wakati huohuo, kocha wa muda wa Chelsea, Guus Hiddink amesema angependa kubaki katika klabu hiyo kama kocha Conte atamhitaji.
Conte na Hiddink
Mdachi huyo alisema: “Nimefanya
kikao kifupi na kocha huyo kuhusiana na mambo mengi yakiwamo soka, kuhusu
Italia, mambo mengine ya nyuma.. kuhusu klabu na kazi tulizowahi kufanya miezi
michache iliyopita. “Napenda kuwa wazi, pindi ninapoingia katika hatua nyingine, kama mtu anataka kupata baadhi ya taarifa, anaweza kuzipata.
“Nimemwambia, kama atanihitaji, ninapatikana kwa ajili ya klabu. Hilo pia nililisema kwa klabu ni kwa sababu naipenda sana klabu hii.”
Post a Comment