MADRID, HIPSANIA
CRISTIANO RONALDO atapatiwa matibabu
maalumu kuweza kutibu jeraha lake ili aweze kucheza mchezo wa marudiano dhidi
ya Manchester City Jumatano ijayo. Nyota huyo wa Real Madrid alikosa mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya uliopigwa Jumanne na kuisha kwa sare ya bila ya kufungana kutokana na majera ya paja.
Awali, ilitarajiwa Ronaldo angecheza mchezo huo baada ya kupumzishwa wiki iliyopita katika mchezo wa Ligi ya La Liga dhidi ya Rayo Vallecano lakini alijitonesha katika mazoezi ya Jumatatu.
Ronaldo, 31, alipata tatizo hilo katika dakika za mwisho za mchezo wa ligi dhidi ya Villarreal, hata hivyo Madrid ilisema ni tatizo dogo.
Picha za zilizoskaniwa jijini Manchester zilionesha kwamba asingweza kucheza dhidi ya Man City - ingawaje Ronaldo alilalamika kutaka kucheza na uamuzi huo ulichukuliwa katika dakika za mwisho.
Mreno huyo amerejea katika mji mkuu wa Hispania na atapatiwa matibabu ili kuweza kutibu majeraha yake.
Bila shaka, atakosa mchezo mwingine wa La Liga dhidi ya Real Sociedad utakaopigwa Jumamosi ingawaje pia kuna wasiwasi kama anaweza kucheza dhidi ya Man City wiki ijayo.
Wasiwasi mkubwa umetawala kwa timu ya madaktari ya Madrid kwamba Ronaldo anaweza kubaki kwenye benchi uwanjani Bernabeu –ambapo itakuwa ni faraja kubwa kwa kocha Manuel Pellegrini na kikosi chake.
Timu ya madaktari watamfanyia uchunguzi Jumatano ijayo kabla ya mchezo- na bosi, Zinedine Zidane atafanya uamuzi wa mwisho wa kumjumuisha katika mchezo huo au la.
Matibabu atakayoyapata Ronaldo ni kama yale aliyoyapata mchezaji wa tenisi, Rafael Nadal baada ya kupata majeraha ya goti.
Sampuli ya seli kutoka kwenye damu ya nyota huyo au uboho itaingizwa katika jeraha na kusambazwa ili kumfanya apone haraka.
Ronaldo amefunga mabao16 katika michezo 10 ya Ligi ya Mabingwa mpaka sasa katika msimu huu.
Mshindi wa mchezo huo atacheza fainali jijini Milan Mei 28 dhidi ya Atletico Madrid au Bayern Munich.
Post a Comment