MUNICH, UJERUMANI
BAYERN MUNICH imelalamikia baadhi ya
maamuzi ambayo yameisaidia Atletico Madrid kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa
Ulaya, kilio hicho kimeshushwa na Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Karl-Heinz
Rummenigge.Ikicheza katika uwanja wake wa nyumbani wa Allianz Arena Jumanne iliyopita, Bayern ilishinda mchezo huo wa pili kwa mabao 2-1 lakini Atletico ilisonga mbele kwa bao la ugenini lililofungwa na Antoine Griezmann.
Lilikuwa shambulizi la kushtukiza baada ya Fernando Torres kumpasia Griezmann aliyechomoka na kuwazidi mbio mabeki wa Bayern na mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa, kumuacha David Alaba na kumchambua kipa Manuel Neuer.
Rummenigge alisema anaamini Griezmann alikuwa amezidi wakati Torres alipokuwa akimpigia pasi, na pia alizungumzia penalti iliyopewa Atletico ambayo Torres aliikosa.
"Tumeona chembembe za udanganyifu," Rummenigge alisema baada ya mchezo.
"Mfungaji wa bao la Atletico alikuwa amezidi, na faulo aliyosababisha penalti (ambayo Atletico ilikosa)ilitokea nje ya boksi. Mwamuzi alichezesha mechi mbili ndani ya siku saba. Sidhani kama watu wa Uefa wanaweza kuwa na mechi nyingi kiasi hicho. Mjumbe wa Uefa aliniambia: “ “Kitendo alichokifanya ni cha aibu."
Post a Comment