MADRID,
HIPSANIA
DIEGO
MARADONA amefunguka mambo mazito na kudai ubaguzi katika soka unamkandamiza beki
wa kati wa Napoli, Msenegali, Kalidou Koulibaly.
Pia Maradona
anamanini klabu yake hiyo ya zamani (Napoli) haiwezi kufanya vizuri katika Ligi
ya Serie A kwa sababa mabingwa wapya, Juventus wanabebwa na waamuzi.
Maneno yenye utata ya Maradona
hayakumuacha kocha wa zamani wa Juve anayehamia Chelsea, Antonio Conte, ambaye
mchezaji huyo mkongwe anaamini amefanya uamuzi wenye mashaka wa kwenda England.Gwiji huyo alifunguka hayo alipokuwa akifanya mahojiano katika runinga moja ya Hispania.
Maradona alikuwa na hamu ya kuweka wazi kile anachoamini ni mtazamo wa kumdhulumu beki huyo mwenye umri wa miaka 24.
“Kama Koulibaly angekuwa Mzungu angekuwa anaichezea Real Madrid au Barcelona. Ubaguzi bado upo katika soka. Wachezaji weupe wanapewa kipaumbele kuliko weusi- na hii haikubaliki.”
Koulibaly iliripotiwa alikuwa akitazamwa na Chelsea akiwa na uwezekano wa kusajiliwa na Conte. Pia, ripoti kama hiyo inasema Manchester United na Bayern Munich zimeonesha kumtamani.
Koulibaly.
Maradona
pia aliigeukia Juventus, ambapo klabu hiyo ya Turin inakimbilia kutwaa taji la
ligi: “Juventus ina wachezaji wazoefu, lakini pia ina waamuzi wa Italia! Hakuna
kitu kipya, wakati kuna wasiwasi kwamba wachezaji wa Juve kila wakati wako
sahihi.”“ Rais wa Napoli, De Laurentiis anapaswa kufanya mambo ili aheshimike, anatakiwa kufanya kile ambacho wakurugenzi wa Napoli walikifanya siku za nyuma.”
Mashambulizi yake juu ya Juve pia yalimhusisha kocha wa zamani wa klabu hiyo Conte.
Maradona hajavutiwa na uamuzi wa Muitaliano huyo kuiacha timu ya taifa na na kuhamia Ligi Kuu: “Kocha wa timu ya taifa ya Italia anahamia Chelsea! Hii naiona ni aibu.”
Post a Comment