MADRID,
HISPANIA
KOCHA
wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesema, straika wake wa Real Madrid, Cristiano
Ronaldo hatacheza mchezo wa Ligi ya La Liga Jumamosi dhidi ya majirani zao, Rayo
Vallecano, lakini kuna wasiwasi mkubwa anaweza
kuukosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City kutokana na
kuumia misuli.
Ronaldo amepatwa na tatizo la misuli
katika dakika za mwisho za mchezo dhidi ya Villarreal Jumatano iliyopita ambapo
timu yake ilishinda mabao 3-0.Uwezekano wa Mreno huyo kucheza Mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya nusu fainali ya kwanza Jumanne ijayo dhidi ya Manchester City bado iko shakani.
Ronaldo alitoka katika mchezo huo akiwa anachechemea baada ya kuumia.
Zidane akimwangalia kwa uchungu.
Baada ya kuchukulikuwa vipimo
Alhamisi na Ijumaa katika mji mkuu wa Hispania, Madrid imesema, Ronaldo mwenye
umri wa miaka 31alikutwa na tatizo la misuli katika mguu wa kulia bila ya
kusema ni lini ataweza kurudi uwanjani.Kocha huyo wa Blancos amezungumza na waandishi wa habari Ijumaa katika mkutano na kudai kwamba, Ronaldo atapewa uangalizi wa karibu, kwa kuwa Madrid iko katika mbio za ubingwa wa Liga na straika huyo anafukuzia kiatu cha mfungaji bora katika ligi hiyo, hata hivyo, hatacheza Jumamosi.
"Kesho (Ronaldo) hatacheza," Zidane alisema. "Tumemfanyia vipimo na hajaumia sana, lakini hataweza kucheza kesho. Tutamwekea uangalizi wa karibu. Kesho atabaki nyumbani. Kisha tutaangalia kuhusu Jumanne."
Zidane alikiri baada ya mchezo wa Jumatano kwamba alitaka kumpumzisha Ronaldo kwa kuhofia majeraha, lakini ilikuwa ni vigumu kwa kuwa straika huyo anataka kucheza kila mchezo.
"Labda
anaweza kupumzika siku nyingine, lakini ni kitu kizuri, mchezaji ambaye kila
siku anataka kucheza, kuisaidia timu, kila siku anataka kupata zaidi na zaidi,"
alisema.
...akifanya vitu vyake.
"Kwa
kocha hilo ni jambo kubwa. Ndani ya mambo mabaya kuna mengi mazuri. Amekuwa
katika wakati mzuri. (majeraha) lilikuwa ni tukio la kipekee, katika dakika za
mwisho chochote kinaweza kutokea. Lakini nimemuona yuko vizuri, kucheza muda wote. Kila
wakati amefanya hivyo. Kwa kocha ni vizuri kuwa na mtu kama huyo. Nifakiria kwa
upande wa faida-kile tunachokipata katika timu."
Post a Comment