LIVERPOOL,
ENGLAND
BEKI wa
Liverpool, Mamadou Sakho amewekwa chini ya uchunguzi kutokana na kufeli vipimo
vya dawa za kuongeza nguvu.
Sakho
anaweza kufungiwa miezi sita baada ya kugundulika akitumia dawa zilizopigwa
marufuku kwa lengo la kupunguza uzito katika mchezo wa pili wa Europa League dhidi
ya Manchester United Machi 17.
Sakho, 26,
atafanyiwa tena vipimo mapema wiki ijayo ili kuthibitisha kama amefeli kwenye
vipimo hivyo.
Pamoja na habari hiyo, Liverpool haijatoa
taarifa ya kumsimamisha mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa ingawaje hatacheza
katika mchezo dhidi ya New Castle United, Jumamosi.
Sakho kazini...
Ripoti zimesema, Sakho binafsi amekuwa
akitumia dawa za kupunguza mafuta na aligundulika katika mchezo huo wa Europa
League. Na Liverpool imetoa taarifa iliyosema: "Jana, (Ijumaa, Aprili 22, 2016, taarifa ya Uefa ilitukifikia ikisema kwamba wako kwenye uchunguzi na kuna uwezekano sheria za utumia wa dawa za kuongeza nguvu zimevunjwa na Sakho.
...akifunga bao
"Mchezaji huyo atawajibika kwa
Uefa kuhusiana na suala hilo na hatahusishwa na kifungo chochote kwa sasa. "Hata hivyo, katika hitimisho, klabu imeamua wakati hatua za uchunguzi zikiendelea, Sakho hatapangwa katika michezo ya Liverpool na hakutakuwa na taarifa zaidi kwa muda huu."
Inafahamika kwamba majibu ya damu ya Sakho, yanatarajiwa kuwekwa hadharani Jumanne.
...akisherehekea
Mwaka 2011, beki Kolo Toure alifungiwa
miezi sita kwa tukio kama hilo alipokuwa akiitumikia Manchester City- ambapo
alidai kwamba alituimia kimamosa dawa za mke wake.
Post a Comment