0


MADRID, HISPANIA
SERGIO Ramos wamewapiga kijembe mahasimu wao Barcelona kwa kuwaambia kwamba kama angefahamu Real Madrid itashinda mechi yake wakiwa pungufu uwanjani basi angetoka kwa kadi nyekundu mapema kabisa.

Pique
Ikicheza pungufu, Real Madrid iliichapa Barcelona 2-1 kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Nou Camp katika mchezo wa La Liga uliofanyika juzi Jumamosi. Mechi hiyo, Barca ilitangulia kufunga, lakini Madrid ilitokea nyuma na kushinda huku ikiwa pungufu baada ya Ramos kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.

Mascherano akikwatua Bale
"Kama ningefahamu mapema kile kilichotokea baada ya sisi kuwa pungufu uwanjani, kwamba tutashinda licha ya kadi nyekundu, basi ningefanya makosa ya kutolewa kwa kadi nyekundu katika dakika ya tano tu," alisema.
Ushindi huo ni kama kisasi kwa Real Madrid ambayo katika mchezo wa raundi ya kwanza ya ligi hiyo uliofanyika kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu ilikubali kichapo cha mabao 4-0 Novemba mwaka jana.

Benzema akifurahia bao
Hata hivyo, Barcelona bado inaongoza ligi hiyo kwa kukusanya pointi 76, saba zaidi ya Real Madrid inayishika nafasi ya tatu kwenye msimamo. Real Madrid iliifunga Barcelona mabao 2-1 Jumamosi uwanjani Camp Nou na kushinda mchezo  El Clasico na kumaliza rekodi ya wapinzani wao hao ya kucheza michezo 39 bila kufungwa.

kadi ya njano
Gerard Pique aliipa Barca bao la kuongoza kabla ya Karim Benzema kuisawazishia Real, na pamojana Sergio Ramos kutolewa kwa kadi nyekundu, Ronaldo aliipatia timu yake bao la ushindi.
Huu ni ushindi wa kwanza wa Madrid dhidi ya  Barcelona tangu mwaka 2013 na kipigo cha kwanza cha  Blaugrana (Barcelona) tangu Oktoba 3.

Makocha wa Real Madrid na Barcelona
Barcelona ilikosa nafasi ya kuongoza katika dakika ya 10, baada ya Neymar kumpa pande Luis Suarez, lakini Suarez hakuweza kuujaza vizuri mpira kwenye mguu wake na kulifanya shuti lake kutoka nje ya lango.
Real Madrid ilijibu shambulio hilo kupitia kwa Gareth Bale alipokimbia na mpira na kuingia nao ndani ya penalti boski na kujaribu kupiga pasi kwa mchezaji mwenzake lakini uliokolewa na Pique.

Post a Comment

 
Top