LONDON, ENGLAND
NEYMAR ameongeza uvumi zaidi kwamba anaweza kutua kuitumikia Ligi Kuu
England baada ya kuhudhuria sherehe za Tuzo za PFA. Staa wa Leicester, Riyad Mahrez alitangazwa kuwa mchezaji bora kwa kushinda tuzo hizo.
Lakini staa huyo wa Barcelona alivuta hisia za watu wengi baada ya kuonekana akiondoka katika klabu ya usiku yenye hadhi ya nyota tatu, Libertine akiwa na Mkurugenzi, Niall Horan.
Mbrazili huyo alipewa siku mbili za mapumziko na bosi wake wa Nou Camp, Luis Enrique baada ya Barca kurejea kileleni kwa kuifunga Sporting Gijon mabao 6-0.
Fununu zimejaa kwamba, Barcelona iko
tayari kumwachia staa huyo aondoke. Na kwa muda sasa Man United imetajwa
kumwania Mbrazili huyo ambaye inadaiwa wawakilishi wake wamekuwa tayari
kutimiza matakwa ya mkataba wake Barcelona kwa kulipa Pauni milioni 144.
Man United pia iko tayari kumpa Neymar mshahara
wa Pauni 300,000 kwa wiki kama atatua Old Trafford. Mbrazili huyo analipwa Pauni 77,000 kwa wiki
na Barcelona.
Mipango ya Man United kumnasa Neymar inaweza kupotea
hewani kama itashindwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Mpaka sasa United inashika nafasi ya
tano ikiwa nyuma ya Arsenal na Manchester
City.
Barcelona nayo iko katika wakati mgumu
kuweza kuwalinda mastaa wake kutokana na mahitaji yao, mbali na Neyma pia inao
wachezaji wengine mashahuri, Messi na Luis Suarez.
Post a Comment