0


LONDON, ENGLAND
KELECHI IHEANACHO, mabao yake mawili dhidi ya Stoke yamemfanya kuwa juu ya vinara wakiwemo Cristiano Ronaldo na Lionel Messi,
Mabao 11 ya kusisimua ya  mchezaji huyo wa Manchester City katika msimu huu, yamekuja katika kiwango cha ajabu katika dakika 81.3 mbele ya Luis Suarez (83.8)
Kocha wa Man City, Manuel Pellegrini ameonekana kuwa na matumaini makubwa na kinda huyo wa kimataifa Nigeria ,19, baada ya kuamua kutonunua straika mwingine wa kumsaidia Sergio Aguero na Wilfried Bony.

Iheanacho
Iheanacho alionwa katika maandilizi ya msimu na kumshawishi Pellegrini kuamua kutoliziba pengo la Stevan Jovetic.
Straika huyo kinda alionesha matunda ya uamuzi huo- alipofunga bao la dakika 89 dhidi ya Crystal Palace na kufunga mara nne katika michezo mitatu ya Kombe la FA.
Kwa upande mwingine Manchester United, Marcus Rashford na Anthony Martial wameshindwa kuirudisha United katika mstari.
Kinda nyota wa England, Rashford ana wastani wa dakika 156 katika ufungaji wa mabao- ingawaje amekuwa akilazimishwa kupewa majukumu makubwa pale Wayne Rooney alipokuwa nje.

...akifanya vitu vyake
Lakini Iheanacho amekuwa kinara kwa kufunga mabao ya kushangaza na kuwa kinara barani Ulaya.
Hakuna mchezaji mwingine wa Ligi Kuu England aliyekuwa na uwiano mzuri wa kufunga mabao kama wake.
Sergio Aguero hajafunga kama ilivyokuwa kawaida yake kwenye ligi na hata katika mashindano ya UIaya.
Lakini Gareth Bale (106.4) anaweza kufikia kiwango hicho baada ya kufurahia msimu mzuri akiwa na Real Madrid, pamoja na kupachika mabao mawili ya kusawazisha dhidi ya Rayo Vallecano.
Ronaldo (84.4)alikuwa nje ya mchezo huo lakini anatarajiwa kurejea dhidi ya Man City katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali jijini Manchester.
Zlatan Ibrahimovic (88.5) pia amepata kura nyingi baada ya  kufunga bao la kuisaidia Paris Saint-Germain.
Straika huyo Msweden anaweza kucheza karata yake England msimu ujao kutokana na mkataba wake na PSG kumalizika mwishoni mwa msimu.

Manchester United imekuwa kihusishwa na uhamisho wa Ibrahomovic, ingawaje inaaminika itawezekana tu kama Jose Mourinho atakuwa kocha wa kikosi hicho na Louis van Gaal akionekana kupendelea zaidi vijana.
Neymar ni peke yake katika safu maarufu ya Barcelona ‘MSN’ aliyekosekana katika 12 Bora ya wafungaji wenye wastani mzuri, wakati Karim Benzema akiungana na wachezaji wenzake Bale na Ronaldo kuipa ushindi miamba ya Madrid.

Post a Comment

 
Top