MANCHESTER, ENGLAND
JOSE MOURINHO atapewa Pauni 300 milioni
kwa ajili ya kufanya usajili mpya pindi atakapotangazwa rasmi kuwa bosi wa
Manchester United.
United itamtangaza Mourinho kuwa
kocha wao mpya baada ya wiki mbili baada ya kusaini dili la kuchukua nafasi ya Louis
van Gaal.Awali kulikuwa na taarifa kwamba Man United inasubiri hadi mwishoni mwa msimu kutoa tamko kuhusu kuachana na Van Gaal na kufanya kazi na Mourinho.
Lakini imekuwa ikilazimisha kutangaza mapema kufuatia habari za Mourinho kusaini mkataba kuvuja nyumbani kwa kocha huyo, Ureno.
Mabosi wa United wanaamini Mourinho ni mtu pekee katika dunia ya soka anayeweza kushindana na Pep Guardiola, ambaye atachukua kibarua cha kuifundisha, Manchester City msimu ujao.
Kwa kuamini hivyo, mabosi hao wa ngazi za juu Old Trafford wamemuahidi Mourinho kiwango kikubwa cha pesa Pauni 300 milioni kuijenga upya timu hiyo.
Kiasi hicho kinaweza pia kumjumuisha, Zlatan Ibrahimovic, ambaye yuko tayari kujiunga na United lakini hataki kucheza chini ya Van Gaal.
Ibrahimovic na Van Gaal waliwahi kufanya kazi pamoja Inter Milan.
Mourinho alifukuzwa Chelsea Desemba mwaka jana na amekuwa akitajwa mara kwa mara kuchukua mikoba ya kuinoa Manchester United badala ya Van Gaal ambaye indaiwa timu imemshinda.
Post a Comment