0


LONDON, ENGLAND
JOSE MOURINHO amefunguka kwamba hana kazi na hana mkataba wowote wa kazi na isipokuwa ana uhakika wa kuanza kazi kabla ya Ligi Kuu England kuanza hapoAgosti.
Mreno huyo amekuwa nje ya kazi yake ya ukocha  tangu alipofukuzwa kazi Chelsea kwa mara ya pili, Desemba, na amekuwa akihusisha na Manchester United.

Mourinho
Louis van Gaal amebakia katika nafasi hiyo Old Trafford na kumekuwa hakuna taarifa yoyote kutoka katika klabu hiyo kama kutakuwa na mabadiliko, lakini tetesi zinaendelea kumhusisha Mourinho na kibarua hicho.
Hata hivyo, Mourinho ambaye alikataa ofa ya kuifundisha timu ya taifa ya Syria alisema yuko tayari kurudi kufundisha soka baada ya msimu huu kufika mwisho.
Mourinho alisema: “Van Gaal ni rafiki yangu, nimefanya naye kazi miaka michache iliyopita. Kila siku nimekuwa nikihusishwa na kazi kadhaa. Mwishoni mwa msimu nitakuwa na kazi, lakini kwa sasa ninaweza kuwaahidi kuwa sina mkataba na klabu yoyote.”
Kuhusu suala la Syria, Mourinho alisema: “Shirikisho la Syria lilitangaza ofa katika mtandao wakamtumia barua wakala wangu. Hilo ninakiri ni kweli, lakini tuliwajibu kwa ustaarabu kuwa hatukuwa tayari kwa kazi hiyo.
“Nimeamua kuliweka hili wazi kwenu (vyombo vya habari) kwa sababu sijazungumza kwa muda mrefu, lakini ninarudi katika nafasi ileile. Kitu pekee ninachoweza kusema sina mkataba na klabu yoyote lakini nitarudi kazini baada ya msimu huu kumalizika.”
                      ...akiwa na kombe la Ligi Kuu England.
Kuondoka kwa mara ya pili kwa Mourinho ndani ya klabu ya Chelsea kumekuja baada ya kushindwa kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ambalo likiwa ni taji la tatu la kocha huyo katika Ligi Kuu.
Kocha huyo amehusishwa na kazi karibu dunia nzima tangu alipoondoka Chelsea, lakini aliweka wazi kwamba anapendelea kufanya kazi katika Ligi Kuu England.
Mourinho mwenye umri wa miaka 53 aliongeza: “Siko katika nafasi ya kukataa kufanya kazi. Niko katika nafasi ya kufanya uamuzi. Hii ni Aprili, kila kitu kitaanza Julai, kila uamuzi utafanywa kati ya Mei na Juni.
“Siko katika nafasi ya kukata tamaa, ninapatikana kwa klabu yoyote, timu ya taifa, lakini natakiwa kuwa mkweli, kama itawezekana ni nahitaji kufundisha klabu.
“Ninapendelea kubaki England. I Ninaipenda nchi, soka linalochezwa hapa, familia yako iko makini na furaha.”

Post a Comment

 
Top