LONDON, ENGLAND
JOSE MOURINHO alikuwa
mmoja wapo kati ya watu wa kwanza kumpongeza bingwa mpya wa dunia wa IBF, Anthony
Joshua kufuatia ushindi wake dhidi ya Charles
Martin.
Bosi huyo wa zamani
wa Chelsea alikuwa shuhuda wakati
bondia huyo Muingerza alipomwangusha
mara mbili bingwa wa zam,ani Martin katika raundi ya pili na kutwaa taji la IBF.
Baada ya pambano
hilo, Mourinho alikuwa nyuma ya jukwaa kumsalimia Joshua na alirudi naye hadi
katika chumba chake cha kubadilishia nguo na kuendelea na kusherehekea ushindi.
Watu wote maarufu
waliokuwepo katika Ukumbi wa O2 Arena walimtakia heri Joshua baada ya kushinda
taji lake la kwanza la dunia.
Baadhi ya mastaa
wengine mbali na Mourinho waliokuwepo
katika ukumbi huo ni Andros Townsend, nahodha wa West Ham, Mark Noble. Mwenyekiti
wa West Ham David Sullivan alikuwapo sambamba na mwigizaji Tamer Hassan.
Straika wa Watford, Troy
Deeney na Scoott Sinclair wa Aston Villa,
mchezaji wa zamani wa Liverpool, Jamie Redknapp alikuwapo sambamba na
mchekezaji, Jack Whitehall.
Hata hivyo alikuwa ni kocha huyoa aliyeipa ubingwa wa Ligi Kuu Chelsea msimu uliopita alialikwa kusherehekea na bingwa huyo mwenye umri wa miaka 26.
Hata hivyo alikuwa ni kocha huyoa aliyeipa ubingwa wa Ligi Kuu Chelsea msimu uliopita alialikwa kusherehekea na bingwa huyo mwenye umri wa miaka 26.
Picha zilimwonesha
Mourinho akiwa na bondia huyo katika chumba cha kubadilishia nguo, na Mreno
huyo akiushika mkanda wa ubingwa wa Joshua
.
Post a Comment