0


LONDON, ENGLAND
JOSE MOURINHO ameitaka Manchester United kuandikishiana naye kama atakuwa kocha mpya wa kikosi hicho mwishoni mwa msimu huu.
Kocha huyo maarufu  kwa jina la ‘Special One’ anaamini itakuwa fedheha kubwa kama hatakuwa kocha wa klabu hiyo.
Lakini kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson anadaiwa kuwa chanzo cha Mourinho kutaka kuandikishiana na Man United.
Ferguson alisema hadharani kwamba anamuunga mkono bosi wa sasa Louis van Gaal wiki iliyopita, huku akiiacha kambi ya Mourinho ikiingiwa na hofu kwamba mambo yanaweza kubadilika.
Hiyo ndiyo sababu inayomfanya Mourinho kutaka kuhakikishiwa kibarua hicho kwa maandishi, kwani anaweza kuanza kazi na mipango ya baadaye ya Old Trafford.
Kuna msuguano mkubwa ndani ya Bodi ya Manchester kuhusu kuchaguliwa kwa Mourinho.
Lakini wamiliki wa Man United, Familia ya Glazer, na Mtendaji Mkuu na Makamu Mwenyekiti wa  Man United, Ed Woodward wanajua kwamba siyo mtu anayeweza kuwafanya warudi kileleni.

Van Gaal
Mourinho kwa sasa hana kazi  tangu alipofukuzwa kazi Chelsea Desemba mwaka jana na amekaririwa kwamba ataanza kazi mwishoni mwa msimu huu.
Hivi karibuni kocha Van Gaal alidai kwamba atamalizia mkataba wake wa msimu mmoja kama alivyokubaliana na Man United bila ya wasiwasi.
Kwa mtazamo huu, itakuwa Mourinho hakuwahi kuingia mkataba wa awali na United kama ilivyodaiwa awali.



Post a Comment

 
Top