LONDON, ENGLAND
ANTONIA CONTE ataingiza Pauni Pauni 6.5 milioni kwa msimu
atakapoanza kazi Chelsea baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu kutoakana na
kipato hicho, atashika nafasi ya tano kwa kulipwa zaidi katika Ligi Kuu
England.
Kocha, Jose Mourinho alikuwa akipata Pauni 13.2 milioni
alipokuwa Chelsea, lakini Pep Guardiola atapata zaidi ya kiasi hicho, akijiunga
na Manchester City mwishoni mwa msimu, kocha huyo ataingiza Pauni 15 milioni
kwa mwaka .
Je, unaulinganishaje mshahara wa Conte na makocha wengine wa
Ligi Kuu England? Hapa chini tunakuletea
kile wanachokipata makocha wanaofundisha ligi hiyo kwa mujibu wa taarifa
zilivyopatikana hivi karibuni bila ya kujumisha bonasi zao.
Arsenal, Arsene Wenger – Pauni 8.3 milioni
Kocha huyo wa Arsenal anaingiza Pauni 8.3 milioni na mkataba wake unafikia
kikomo 2017.
Aston Villa, Remi Garde – Pauni 2 milioni
Kocha wa Aston Villa, Eric Black anapata sawa kama
mtangulizi wake, Tim Sherwood ambaye alikuwa akipata Pauni 2 milioni kwa mwaka
kabla ya kufukuzwa.
Bournemouth, Eddie Howe-Pauni 750,000
Bournemouth pamoja na kwamba hali ya hewa imechafuka na kuwa
katika harakati za kupambana kutoshuka daraja. Kwa sasa iko nafasi ya 18, bado
kocha wake analipwa Pauni 750,000 pamoja na matatizo yake.
Chelsea,
Antonio Conte – Pauni 6.5 milioni
Conte atachukua Pauni 6.5 milioni kwa mwaka. Muitaliano huyo
atapata bonasi ya Pauni 5 milioni kama ataweza kutwaa Kombe la Ligi ya Mabingwa.
Crystal Palace, Alan Pardew- Pauni 1.5 milioni
Crystal Palace inajaribu kujiondoa katika hatari ya kushuka
daraja na kocha wake, Pardew anaingiza Pauni 1.5 milioni kwa mwaka.
Everton, Roberto Martinez – Pauni 3 milioni
Martinez aliahidi kuipeleka timu hiyo katika Ligi ya
Mabingwa Ulaya wakati alipowasili Everton, lakini sasa anatimiza mwaka wa nne
wa mkataba wake wenye thamani ya Pauni 3 milioni, akiwa bado hajatimiza ahadi yake.
Leicester City, Claudio Ranieri – Pauni1.5 milioni
Leicester City, Claudio Ranieri – Pauni1.5 milioni
Kuna uwezekana akatwaa ubingwa mwishoni baada ya raundi sita
zijazo na anaingiza Pauni 1.5 milioni kwa mwaka. Hata hivyo, Ranieri anajiopanga
kuzawadiwa mshahara wake mara mbili mwishoni mwa msimu.
Liverpool, Jurgen Klopp – Pauni 7 milioni
Brendan Rodgers, iliaminika kwamba alikuwa akilipwa nusu ya
Pauni 7 milioni kwa mwaka. Lakini Mjerumani, Jurgen Klopp analipwa kiasi hicho
kizima.
Manchester City, Pep Guardiola – Pauni 15 milioni
Guardiola ataondoka Bayern Munich mwishoni mwa msimu
huu na kujiunga na Manchester City, ambayo
itamlipa Pauni 15 milioni kwa mwaka. Inadaiwa kocha wa sasa Manuel Pellegrini hapati
hata nusu ya kiasi hicho.
Manchester United, Louis van Gaal –
Pauni 7.3 milioni
Van Gaal analipwa Pauni 7.3 milioni lakini kama kocha Jose Mourinho
atachukua nafasi yake mwishoni mwa msimu kama inavyodaiwa, atadai malipo
yanayokaribia na yale aliyokuwa akilipwa Chelsea, Pauni 13.2 milioni.
Newcastle United, Rafa Benitez – Pauni 4 milioni
Benitez anashikishwa Pauni 4 milioni kwa mwaka katika mkataba
unaomtaka kuifufua Newcastle hata kama kuna
kifungu katika mkataba wake anaweza kuondoka kama timu itazidi kushuka.
Norwich City, Alex Neil – Pauni 750,000 milioni
Neil anajaribu kuilinda Norwich kusonga mbele katika mikono
salama na inafahamika kwamba anachukua mshahara sawa na anaupata Howe wa
Bournemouth.
Southampton, Ronald Koeman- Pauni 2 milioni
Mkataba wa Kocha Koeman unafikia kikomo lakini kocha huyo wa
Southampton hajafanya uamuzi kama ataendelea kuwepo St Mary hadi mwishoni mwa
msimu. Kwa sasa anaingiza Pauni 2 milioni.
Stoke City, Mark Hughes – Pauni 1 milioni
Hughes inasemekana analipwa Pauni 1milioni kwa mwaka
uwanjani Britannia huku klabu hiyo ikiwa katika nafasi ya nane hadi sasa.
Sunderland, Sam Allardyce – Pauni 3 milioni
Allardyce anajaribu kuisogeza sehemu salama Sunderland na
amekuwa akipata karibu Pauni 3 milioni
kwa mwaka kwa kufanya kazi hiyo.
Swansea City, Francesco Guidolin – Pauni 1milioni
Pamoja na kutowekewa bonasi ya kukiokoa kikosi hicho,
Swansea inamlipa Guidolin Pauni 1milioni.
Mkataba wake utahitajika kutazamwa upya mwishoni mwa msimu.
Tottenham Hotspur, Mauricio Pochettino – Pauni 3.5 milioni
Tottenham inapambana kusaka ubingwa ikiwa inaifukuza Leicester
huku kocha wake, Pochettino akichukua Pauni 3.5m baada ya kumwaga wino katika
dili la miaka mitano mwaka 2014.
Watford, Quique Sanchez Flores - Pauni1milioni
Slavisa Jokanovic alitaka kulipwa Pauni 2.5 milioni lakini, Watford
ilikataa na kutaka kumpa Pauni 1milioni, aliachana nayo.
Klabu hiyo ikarudi tena kwa Flores ambaye alikubali dau hilo.
West Bromwich Albion, Tony Pulis – Pauni 2 milioni
Pulis inadaiwa amehitaji kulipwa Pauni 2 milioni kwa mwaka
ili aweze kuwa bosi mpya wa West Brom na inasemekana klabu hiyo imekubaliana
naye.
West Ham, Slaven Bilic – Pauni 3 milioni
Bilic amesaini mkataba wa miaka mitatu Juni 2015, wenye
thamani ya Pauni 3 milioni kwa msimu. Chini yake klabu inapigania kucheza Ligi
ya Mabingwa Ulaya.
Post a Comment