0


MANCHESTER, ENGLAND
LOUIS VAN GAAL ameukataa mpango wa kurudi Uholanzi baada ya Chama cha Soka cha Uholanzi (KNVB) kutaka kumpa nafasi ya ukurugenzi wa ufundi wa timu ya taifa ya nchi hiyo, imethibitishwa.
Wiki iliyopita iliripotiwa kwamba KNVB inataka kumchagua Van Gaal kuwa mkurugenzi wa ufundi katika kituo kipya cha soka cha nchi hiyo kinachotarajiwa kumalizika katika msimu wa majira ya joto.

Mdachi huyo ambaye aliifundisha timu ya taifa ya Uholanzi katika Kombe la Dunia la mwaka 2014 yuko kwenye wasiwasi mkubwa wa kumaliza mkataba wake unaofikia kikomo 2017 huku ikidaiwa kwamba anaweza kuondolewa Man United na nafasi yake kuchukuliwa na Jose Mourinho.
Hata hivyo, inadaiwa kwamba Van Gaal amekataa kurudi kuchukua majukumu ya kimataifa ya Uholanzi baada ya kuhakikishiwa kuendelea kuitumikia Old Trafford msimu ujao.
Mwaka jana, bosi huyo wa United mwenye umri wa miaka 64 alisema kwamba atastaafu kufundisha soka mwaka, 2017 na kumuahidi mke wake kwamba mkataba wa Man United utakuwa wa mwisho kufanya kazi hiyo.

Post a Comment

 
Top