MADRID, HISPANIA
GARETH BALE amefunguka kwamba hajawahi
kuwa na matatizo na mchezaji mwenzake wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo na
anafurahia kuwa chini ya kocha, Zinedine Zidane.Bale, 26, alijiunga na Real Madrid akitokea Tottenham mwaka 2013 katika dili ambalo kwa mujibu wa nyaraka zilizovuja lina thamani ya Euro100.7 milioni, ikivunja rekodi Euro 96 milioni ada iliyolipwa Manchester United kwa Ronaldo mwaka 2009.
Dili hilo liliripotiwa kumkera Ronaldo ikidaiwa kuwa staa huyo wa kimataifa wa Wales amesajiliwa kwa lengo la kuwa mbadala wa kuchukua nafasi yake, na nyota huyo wa Ureno siku za mwanzo alionesha kuchanganyikiwa juu ya straika mwenzake huyo walipokuwa uwanjani.
Ronaldo na Bale
Hata hivyo, Bale amefafanua kwamba
hakuna tatizo kati yake na Ronaldo mwenye umri wa miaka 31."Anazungumza Kiingereza, kitu kilichonisaidia mara ya kwanza nilipofika hapa," alisema.
"Tunamuunganiko kutoka Ligi Kuu. Tuko vizuri kweli. Vyombo vya habari vinazungumza vitu vingi ambavyo labda hatuvijui lakini tuko vizuri.
Bale
"Kamwe hatujawahi kuwa na matatizo.
Sijawahi kugombana naye. Ni mtu mwenye ushirikiano uwanjani- kila mmoja
analijua hilo. Ni mwenye hekima. Watu wakati mwingine wanachukulia mambo sivyo.
Hatujawahi kuwa na matatizo."Aliongeza: "Mara zote mnafanya kazi kwa ushirikiano. Hakuna ayeweza kufanya kila kitu peke yake. Lakini unahitaji ubinfsi kiasi kwa sababu hicho ndicho mtu wa mwisho anatakiwa kuwa nacho.
Alisema Ronaldo "anajitoa kwa kila kitu " uwanjani na kuongeza: "Yeyote anayefunga tunakuwa na furaha. Tunahitaji kushinda mataji."
Bale alipewa jukumu la kuwa mshambualiji wa mwisho wakati wa kocha, Rafa Benitez mwanzoni mwa msimu lakini amekuwa akitumika pembeni tangu alipokuja kocha Zidane Januari.
Bale amekuwa shabiki mkubwa wa Benitez, ripoti zikisema amekuwa akizingatia mustakabali wake wa baadaye baada ya Mhispania huyo kufukuzwa, na Bale alimkubali sana bosi huyo wa zamani wa Liverpool na Chelsea.
"Nilizungumza na Benitez sehemu ninayohitaji kucheza kwa sababu msimu uliopita sikudhani kama nilipata mipira ya kutosha," alisema Bale.
"Nilijihisi nimetengwa katika winga na sikuwa na uwezo wa kufanya kile kitu bora nilichokuwa nataka kuifanyia klabu.
"Alinisikiliza na akanipa majukumu zaidi ambayo nilikuwa nikiyahitaji. Nilikuwa na uhusiano naye mzuri. Anazungumza Kiingereza vizuri kitu kilichonisaidia. Nilikuwa naweza kuzungumza naye vya kutosha. Tulikuwa na vitu mambo ya kawaida kutokana na kufanya kazi England. Nilifurahia kufanya naye kazi."
Hata hivyo, Bale alisema anafurahi kufanya kazi chini ya Zidane, ambaye amekuwa akifanya kazi kama msaidizi wa Carlo Ancelotti wakati msimu wake wa kwanza alipotua Bernabeu, pindi klabu iliposhinda Copa del Rey na Ligi ya Mabingwa.
"Alishinda Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa kama mchezaji na anajua kwa kiasi gani lina maana kwa klabu," Bale alisema kuhusu Zidane, ambaye bao lake liliifanya Real kushinda fainali ya mwaka 2002 dhidi ya Bayer Leverkusen.
Zidane
"Alikuwa ni kocha wa ukweli
tuliposhinda mwaka 2014. Anaijua klabu kuliko yeyote. Hajaondoka klabuni baada ya kustaafu."Bale aliendelea kumwagia sifa Zidane: "Ni mpole. Hata alipokuwa mchezaji, siku zote aliacha soka lake lizungumze. Hiyo inaonesha ni mtu wa aina gani. Kwa sababu alikuwa mchezaji mzuri tunajua atakuwa kocha mzuri.
Post a Comment