0


LONDON, ENGLAND
DIEGO COSTA amefungiwa mchezo mmoja kutokana na hasira baada ya kupewa kadi nyekundu katika mchezo wa robo fainali wa Kombe la FA ambao Chelsea ilifungwa na Everton.
Straika huyo alipandwa na hasira baada ya kuoneshwa kadi ya pili ya njano na mwamuzi, Michael Oliver na kukataa kutoka nje ya uwanja kwa muda.

Hiyo inamaanisha kwamba, Costa hatakuwamo kwenye safari ya wachezaji wa Chelsea watakaokwenda  kupambana na Swansea na vilevile dhidi ya Aston Villa  katika uwanja wa nyumbani wiki hii.

Waraka wa FA ulisomeka hivi: "Kufuatia Tume Huru ya Udhibiti iliyosikiliza shauri hilo, Alhamisi (31 Machi 2016), Diego (Costa) amesimamishwa mechi moja na kupigwa faini ya Pauni 20,000 na kupewa onyo kutokana na tabia yake siku za usoni.
"Costa alikiri kosa hilo la utovu wa nidhamu alilolifanya baada ya kuoneshwa kadi ya pili ya njano katika mchezo wa Kombe la FA raundi ya sita uliofanyika Machi 12, 2016 uwanjani Goodison Park. Adhabu hiyo inaanza mara moja."

Post a Comment

 
Top