LONDON, ENGLAND
RIYAD MAHREZ ameandika jina lake
kwenye vitabu vya historia baada ya kuwa Mwafrika wa kwanza kushinda Tuzo ya
Mwanasoka Bora wa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa (PFA).Nyota huyo wa Leicester amekuwa na msimu mzuri uwanjani King Power baada ya kufunga mabao 17 na kutoa pasi za mabao (asisti)11 katika michezo 34 ya ligi na kuisaidia timu yake kukaribia kushinda taji la Ligi Kuu.
Mahrez
Kwa kitendo hicho Mahrez, 25, anaweza
kuirudisha Afrika kwa mara ya kwanza katika historia ya tuzo hizo.Mchezaji huyo wa kimataifa wa Algeria ni mtu wa pili kuchukua tuzo hiyo nje ya Bara la Ulaya- wa kwanza kufanya hivyo akiwa ni Luis Saurez aliyeshinda mwaka 2014 alipokuwa akiitumikia Liverpool.
...akishangilia
Kumekuwa na wachezaji wengi wa
Kiafrika waliokuwa na uwezo mkubwa na hawakuweza kupewa tuzo hiyo.Kama kina Yaya Toure, Nwanko Kanu na Didier Drogba wote walishiondwa kutwaa tuzo hiyo miaka ya nyuma.
Na hilo linafanya maendeleo ya Mahrez kuwa ni muhimu zaidi baada ya kununuliwa na Leicester kwa Pauni 400,000 kutoka La Havre, Januari 2011.
Mahrez
Leicester ambayo ni maarufu kwa jina
la Mbweha ikiwa chini ya kocha, Claudio Ranieri iliingiza wachezaji wengine
kina Jamie Vardy na Ngolo Kante katika kuwania tuzo hiyo.Na klabu hiyo ya Midland inahitaji kama pointi tano tu katika michezo yao mitatu ya mwisho baada ya kuitandika Swansea mabao 4-0 ili kutwaa taji la Ligi Kuu England katika historia.
Post a Comment