NA PRIVA ABIUD
HIVI karibuni niliandika makala kuhusu James Rodríguez,
nikasema hivi: " Rodríguez, ameongezeka uzito, amepungua kasi
yake, anachelewa mazoezini mara kwa mara.
Kazi yake kubwa ni kukimbiza magari na kukatika
kwenye klabu za usiku. Amesahau, Angel Di Maria na Mesut Ozil wameondoka Real Madrid
na vipaji vyao, je yeye ni nani?
Je, akiondoka ataenda klabu ipi kubwa
zaidi ya Real Madrid? Wapi atapata anachotaka? Wapi atacheza na wachezaji
wakubwa kama Criastano Ronaldo, Gareth Balle na Ton Kroos bila kusahau Luka Modric?
Rodriguez
Lakina baada ya kusema hayo, sikumwacha
Rodríguez, hivi hivi ila nilimpa pia ushauri. Nimkumbushe
Rodríguez, kuwa, kwenye lile begi ambalo
amejifanya amelisahau kwa sababu ni la kishamba, lina mkataba unaonesha
alinunuliwa kwa Euro 80, akumbuke pia ndani yake kuna gazeti alilonunua ili
aone waandishi wanasemaje juu yake.
Gazeti hilo liliandika Madrid imepoteza
pesa kumnunua maana tayari Isco alionesha uwezo.
Isco
Mwambieni mbali na magazeti kumchafua
kote kule lakini msimu wake wa kwanza alionekana bora kuliko Isco, kumbe jitihada
ziliwaambua waandishi kama kina Lucas Leverette na Gonzalo Arroyo. Lakini
sikuishia hapo, pia nilimwambia : Rodríguez, arudi stendi akachukue mabegi yake
aliyoyasahau asome tena vipengele vya mkataba wake halafu ajiulize ni wapi atapata
timu itakayompa mkataaba mnono kama ule!
Mwambieni arudi stendi maana lile begi
litamkumbusha mengi, litamkumbusha wapi alipotoka, na litamkumbusha yeye ni
nani Madrid na anapaswa kufanya nini ili awe Xabi Alonso, ili awe Ike Casilas,
na ajenge jina lake Madrid.
Rodríguez, sijui kama alichukua mabegi yake au la, ila ninachojua
Isco inabidi amsindikize Rodríguez. Nimesmikia Isco akilalamika kuwa yeye
na Rodríguez, wanalalamikiwa kwa matokeo mabovu na viwango
vyao kushuka.
Kuhusu Rodríguez, nilishamsema lakini Isco sijui niseme
nini juu yake! Kwanza isco hajashuka kiwango, tatizo ni aina ya uchezaji wake!
Sio mtu wa kumkabidhi jukumu la kutafuta matokeo, amekuwa mbinafsi, amepewa
mpira mara nyingi zaid ya alivyotoa mpira yeye. Amekosa msimamo anapokuwa na
mpira, yaana niseme ni nyuki wa mashineni. Hawezi kucheza kama Modric, hawezi
kusimama kama Kroos, hawezi kupambana,
Mateo Kovačić hawezi kuzuia kama Casemiro
anacheza yeye kama yeye!
Kocha Zidane
Yaani utadhani anacheza gombania goli.
Hachezi kama Wahispania (one touch) anacheza kama Muargentina (Di Maria, Lionel
Messi, Diego Maradona, Kun Aguero) hawa mpaka watoe pasi labda mbele yao
wamuone Pepe.
Kwa mchezo huu, kocha Zinedine Zidane
hawezi kukupanga.
Utaozea benchi.
Isco jifunze kutoka kwa Ozil kama
hutaki nenda stendi na Rodríguez, mpande basi maana Madrid pamewashinda.
Post a Comment