0


LONDON, ENGLAND
JAMIE VARDY ataukosa mchezo wa Manchester United Jumapili ijayo baada ya Kamati ya Uthibiti kumfungia mchezo mmoja staa huyo wa kimataifa wa England kutokana na utovu wa nidhamu.
Jopo la watu watatu limeamua kwamba kitendo cha hasira cha Vardy kilichosababisha kutolewa nje dhidi ya West Ham kilikuwa kinastahili kupewa adhabu zaidi na kocha Claudio Ranieri atalazimika kumkosa  kinara huyo wa ufungaji katika mchezo wa pili mfululizo. 

Tukio lililomponza, Vardy
Vardy hakuitumikia Leicester City katika mchezo wa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Swansea Jumapili iliyopita, ambapo aliushuhudia mchezo huo akiwa katika jukwaa la watu mashuhuri uwanjani King Power, kabla ya kuhudhuria  Tuzo za PFA jijini London na kufanikiwa kupata tuzo ya kupachika mabao 11 mfululizo katika Ligi Kuu England.
Straika huyo wa Leicester alikaa katika jiji hilo hadi usiku kwa ajili ya kuhudhuria shauri lake uwanjani Wembley Jumatatu, ambapo alitoa ufafanuzi juu ya hisia zake zilizosababishwa na mwamuzi, Jon Moss kumuonesha kadi ya pili ya njano kwa kujirusha.
Vardy alimuonesha kidole Moss na akaapa huku akitegemea rekodi yake ya kutowahi kutolewa nje siku za nyuma katika Ligi ingeweza kumsaidia.
                        ... akihudhuria Tuzo za PFA
Vardy hajawahi kuoneshwa kadi kwa kudanganya ‘kujiangusha’ siku za nyuma katika Ligi Kuu na kocha wa timu ya taifa ya England, Roy Hodgson amedai kitendo hicho ni cha kibinaadamu.

...akipokea tuzo yake
Lakini jopo liliamua kumfungia mechi moja zaidi, ikimaanisha kwamba Vardy ambaye amepachika mabao 22 katika Ligi Kuu  msimu huu, atakuwa nje tena katika mchezo utakaopigwa Old Trafford dhidi ya Manchester United wakati Leicester ikipigania kutwaa taji la Ligi Kuu.
Straika huyo mwenye umri wa miaka 29, pia amepigwa faini ya Pauni 10,000.

... hakuamini kilichotokea.
Diego Costa na Gabriel waliwahi kukutana na adhabu kama hiyo kutokana na makosa kama hayo ya utovu wa nidhamu baada ya kuoneshwa kadi nyekundu msimu huu.
Kocha Ranieri sasa atapambana na Louis van Gaal bila ya kuwa na straika wake muhimu katika  mchezo huo. 

Post a Comment

 
Top