0


LONDON, ENGLAND
EDEN HAZARD amemwonesha ishara bosi mpya wa Chelsea, Antonio Conte kwamba anajiandaa kubaki klabuni hapo kwa ajili ya msimu ujao, chanzo cha karibu kimethibitisha.
Maisha ya baadaye ya Hazard yamekuwa yakitawaliwa na uvumi wa mara kwa mara na kudaiwa kushuka kiwango kwa kiungo huyo msimu huu kumesababisha Chelsea kushindwa kutetea taji lake la Ligi Kuu.

Hazard
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji ameshindwa kung’ara kama ilivyokuwa msimu uliopita, ambapo alishinda tuzo mbili za PFA na FWA, mpaka sasa bado hajafunga bao lolote katika msimu huu wa Ligi Kuu England.
Real Madrid na Paris Saint-Germain zote zimetajwa kumuwinda kiungo huyo, lakini bado ambaye katika mktana wake amebakisha miaka minne.
Conte alizungumza na wachezaji mbalimbali alipotembelea viwanja vya mazoezi ya klabu hiyo baada ya kutangazwa kwamba atakinoa kikosi hicho msimu ujao, mapema mwezi huu, na katika mkutano wake na Hazard, Muitaliano huyo alimwambia anataka abaki Stamford Bridge.

Conte
Chanzo cha karibu na Hazard kimesema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alifurahia matokeo ya mkutano huo na Conte na kumthibitishia bosi huyo mpya wa Chelsea kwamba hana mpango wa kuondoka na anataka kurudisha kiwango chake, kutoa changamoto na  kuisaidia timu kurudisha heshima yake.
Habari za Hazard kuonesha hamu ya kutaka kubaki Chelsea zimekuja kwa lengo la kumkaribisha Conte ambaye anajukumu kubwa la kukijenga upya kikosi cha Chelsea.

Post a Comment

 
Top