0


LONDON, ENGLAND
EMMANUEL ADEBAYOR amekiri kwamba alifanya makosa kulazimisha kuondoka Arsenal.
Straika huyo alipokewa vibaya na mashabiki wa Arsenal aliporudi Emirates Jumapili akiwa na Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu ulioisha kwa sare ya bao 1-1.
Kila alipogusa mpira alikuwa akizomewa na mashabiki wa Arsenal ambao bado hawajamsamehe straika huyo tangu alipohama klabu yao na kujiunga na Manchester City mwaka 2009.

Adebayor anaonekana machoni mwa mashabiki wa Arsenal kama mtu mwenye tabia mbaya kutokana na kitendo chake cha kushangilia alipofunga dhidi ya timu yake hiyo ya zamani katika mchezo wa kwanza dhidi yao Septemba 2009.

Baada ya kubezwa katika michezo yote na kusika kelele kuhusu uhusiano wake mbaya na mama yake, Adebayor alijibu kwa kukimbia umbali wa kiwanja  kushangilia  mbele ya mashabiki wa Arsenal mara baada ya kufunga bao.

Pia, alimpiga teke la uso straika wa zamani wa Arsenal Robin Van Persie katika mchezo huo na alifungiwa michezo mitatu kutokana na kukimbia umbali mrefu kwenda kushangilia  pamoja na kuwachezea rafu Alex Song na Cesc Fabregas.
Adebayor alisema: “Kwangu, mwisho wa siku ninakuwa na furaha kuhusu nilipotoka na nilipo leo- ninapaswa kusahau kuhusu wote wanaonichukia.

“Mashabiki wote wa Arsenal  wananizomea na ninapoangalia nyuma, naelewa ni wapi mambo yalipoenda kombo, lakini katika maisha haya kuna vitu huwezi kuvirudisha nyuma kabisa, unapaswa kuviangalia na kusema, nilifanya makosa.”
“Sote huwa tunafanya mambo kama hayo katika hatua kama hizo za maisha yetu ambayo hatupaswi kuvifanya lakini jambo la muhimu ni kuzidi kusonga mbele.
“Hii siyo mara yangu ya kwanza kuja kurudi kucheza dhidi ya Arsenal uwanjani Emirates.
“Unaweza kuona wakati nilipokuwa benchi, pindi nilipopasha misuli walinizomea, nilikuwa nacheka,”alisema.

Post a Comment

 
Top