NANJING, CHINA
RAMIRES kiungo wa Kibrazili amefunguka
kwamba ameondoka Chelsea na kujiunga na Ligi ya China (CSL) katika klabu ya Jiangsu
Suning kwa sababu ya kocha, Guus Hiddink.Ramires alidumu katika klabu hiyo ya London kwa miaka sita na kucheza mechi 160 na kufunga mabao 17.
Pia, ameshinda mataji matano yakiwemo ya Ligi Kuu, Kombe la FA, Kombe la Ligi, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la Europa League-na alikuwa mchezaji muhimu chini ya kocha aliyefukuzwa Jose Mourinho.
Ramires akiwa na shabiki.
Chini ya utawala wa Hiddink, Mbrazili
huyo ameanza kwenye mchezo mmoja tu, katika Kombe la FA dhidi ya Scunthorpe Januari
10 mwaka huu.Kutokana na kukosa nafasi ya kucheza, kulimfanya Remires kuomba uhamisho wa kushtukiza wa Pauni 25 milioni kujiunga na Jiangsu mwezi Januari, sambamba na Mbrazili mwenzake Alex Teixeira.
"Moja ya sababu kubwa ya kuondoka Chelsea ni kuwasili kwa kocha mpya," Ramires alitoboa.
"Siyo kwa sababu nilikuwa na uhusiano mzuri na Jose (Mourinho). Lakini alipokuwa hajafukuzwa, nilijua nilikuwa na nafasi ya kucheza na nafasi ya kupigania namba kwenye timu ilikuwa wazi.
"Mwishowe alipokuja Hiddink, alinitoa kwenye nafasi bila ya sababu. Sikujua ni kwanini kwa sababu nilikuwa nacheza vizuri na nilipambana kwa ajili ya timu ambayo ilikuwa katika wakati mgumu.
...akiwa mazoezini na wachezaji wenzake.
"Hakunipenda kama mchezaji au kwa jinsi nilivyo na kuamua kutonipa nafasi ya kupigania namba katika timu.
"Hata baada ya kucheza dakika 90 dhidi ya Scunthorpe, mechi iliyofuata ya Ligi Kuu sikuhusishwa. Nilikaa katika benchi hadi mwisho wa mchezo na baada ya hapo sikuwa hata katika wachezaji wa akiba.
"Nilikaa kwa muda mrefu bila ya kucheza pale na nilihitaji kuungana na timu na kuisaidia kwa kuwa haikuwa katika wakati mzuri. Na haikuwa rahisi kuangalia timu ukiwa umekaa katika benchi na kuiona kama inacheza vizuri.
"Ujio wa Hiddink kweli ulimaliza kila kitu changu na sikujua kwanini... lakini nadhani hili ndio soka."
...sasa mambo safi.
Mbrazili huyo alifafanua kwamba
aliamua kujiunga na Jiangsu ili kufufua hamu yake ya kucheza na kulinda nafasi
yake kwenye timu ya taifa ya Brazil."Kwa hiyo nilijiona nikipotea Chelsea. Kwa kweli nilishapotea. Katika mazoezi ya vipindi mbalimbali, nilipambana sana kwa mapenzi, ujuzi na nguvu- lakini haikuonekana kitu katika uwanja wa mazoezi, Cobham.
Post a Comment