0


PARISI, UFARANSA
ANGEL DI MARIA ameanzisha mashambulizi kwa Manchester United chini ya Louis van Gaal akielezea kuondoka kwake klabuni hapo.
Mshambuliaji huyo wa Kiargentina  amesema alikuwa akichezeshwa nje ya nafasi aliyoizoea, kitendo kilichokuwa kikimnyima raha, na ameondoka Man United kwa hiyo anaweza kushinda vitu vingi.

Di Maria mwenye umri wa miaka 28 alinunuliwa na katika kikosi cha Van Gaal Agosti 2014 kwa kiasi kinachokadiriwa kufikia  Pauni 60 milioni lakini baada ya msimu uiskuwa na mafanikio, alijiunga na Paris Saint-Germain mwaka mmoja baadaye kwa dili linalofikia  Pauni 44 milioni.
Di Maria, ambaye alicheza nafasi sita tofauti alipokuwa Man United, alisema: "Siyo vizuri kusema baadhi ya mambo lakini ni kwamba hawakunifanya niweze kukaa vizuri, ndio maana sikukaa.

"Nimeondoka na timu bado inacheza vilevile. Imetolewa katika mashindano ya Ulaya, iko mbali kuweza kuwa bingwa wa Ligi Kuu.
"Sidhani kama ni kutokana na jukumu langu au jukumu la wachdezaji wenzangu. Kila nilkipokuwa nikipewa nafasi ya kucheza, nilifanya kazi nilivyoweza lakini sikufanikiwa kama nilivyotarajia. Kwa hiyo nikaamua kuondoka, siyo tu kwa ajili ya kuwa na furaha, bali pia kwa ajili ya kushinda vitu vingine."
Di Maria alianza vizuri katika michezo yake ya kwanza akiwa na Man United kwa kufunga mabao matatu katika mechi tano. Baada ya hapo, aliongeza bao moja tu katika michezo 27 iliyofuata- dhidi ya Yeovil Town katika Kombe la FA- kabla hajaondoka katika klabu hiyo.

"Nilianza kucheza katika nafasi ya kwanza, kisha katika mchezo mwinguine nikacheza nafasi nyingine. Nilifunga mabao wakati nikicheza katika nafasi moja, kisha ghafla mchezo unaofuata ninaoangwa katika nafasi tofauti. Nadhani hilo halikuwa na msaada kwangu kuweza kuendelea kubaki," alisema.

"Ni juu ya kocha kuamua wapi na vipi kila mchezaji anatakiwa kucheza, lakini nadhani mchezaji anajisikia vizuri kucheza katika nafasi ambayo ameizoea. Hicho ndicho ninachokifanya hapa (PSG) na ninamshukuru kocha wangu kwa hilo."
Alimpongeza kocha wake, Laurent Blanc, kwa kutomwamisha katika nasafi za kucheza uwanjani kama alivyokuwa akifanya Van Gaal.
Di Maria aliongeza: "Kuanzia mwanzo alikuwa akijua wapi natakiwa nicheze na hajabadilisha mawazo yake. Amenipa uhuru mkubwa sana kucheza pale ninapotaka kucheza. Nina furaha hapa na haikuwa kesi zaidi ya hapo.

Post a Comment

 
Top