0


MADRID, HISPANIA
ZINEDINE ZIDANE amesema mchezo wa Jumamosi wa El Clasico wa Ligi ya La Ligi kati ya Barcelona na Real Madrid, uwanjani Camp Nou hauwezi kumyima usingizi na atalala vizuri bila ya kuwa na hofu yoyote.
Madrid inakwenda kwenye mchezo huo ikiwa nafasi ya tatu katika msimamo, ikiwa pointi 10 nyuma ya vinara wa ligi hiyo Barcelona, na timu hiyo ikiwa haijaongezeka kiwango  tangu ilipochukuliwa na Zidane kutoka kwa Rafa Benitez, Januari mwaka huu.

...Zidane akiwa na siraha yake, Ronaldo
Makocha waliomtangulia wa ‘Blancos’ wamepoteza mchezo wao wa  kwanza wa Clasico- Novemba mwaka jana Benitez alifungwa mabao 4-0 katika uwanja wa nyumbani  wa Santiago Bernabeu.
Na mwaka Novemba 2010, Jose Mourinho akiwa katika benchi kwa mara ya kwanza alichezea kichapo cha mabao 5-0 uwanjani Camp Nou.

Zidane alipoulizwa katika mkutano kabla ya mchezo huo kuhusu ni nini kitakachotokea katika mchezo wake wa kwanza akiwa katika benchi kama kocha dhidi ya Barcelona alisema haofii hata kidogo na anajipanga kufurahia mchezo huo.
"Usiku nitalala vizuri tu," Zidane alisema. " Huo ndio ukweli. Ni mchezo wa soka. Tunatakiwa tukumbuke hilo na kufurahia- kucheza dhidi ya wachezaji wazuri na kujipima dhidi ya Barca.
“Nitapata usingizi kama ninavyolala siku zote. Nitafurahia mchezo wangu wa kwanza kati ya Barca na Madrid nikiwa kama kocha. Nataka kufurahia."

Zidane
Jumamosi hii inatimia miaka 10 na siku moja tangu Zidane alipokutana na Barcelona akiwa kama mchezji katika mchezo wa sare ya bao 1-1 uwanjani Camp Nou.
Pamoja na kwamba, Real Madrid inamtegemea Criastiano Ronaldo, Karim Benzema na Gareth Bale safu ya Barcelona inatisha zaidi kwa kuwa na Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar.

Post a Comment

 
Top