WEST
HAM, ENGLAND
ARSENAL
imekata pumzi baada ya kulazimishwa sare na West Ham uwaanjani Upton Park na
kutanua ukubwa wa pointi zake dhidi ya vinara wa ligi hiyo Leicester City.
Mpaka
sasa Arsenal inayonolewa na Mfaransa, Arsene Wenger iko nyuma kwa pointi 11 kutokana
na sare hiyo ya mabao 3-3 katika mchezo mkali wa Ligi Kuu.
Carrol
Katika
mchezo huo, Arsenal ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Ozil na
Sanchez katika dakika ya 18 na 35.
Straika
wa zamani wa Liverpool, Andy Carroll aling’ara katika mchezo huo baada ya
kufunga ‘hat-trick’, alianza kwa kusawazisha mabao hayo katika dakika za 44 na 45 na baadaye kuifungia West Ham bao la
kuongoza katika dakika ya 52.
Ozil akifunga.
Beki
wa kati, Laurent Koscielny aliinusuru Arsenal kupokwa poingi zote tatu baada ya
kusawazisha bao la tatu katika dakika ya 70.
Ozil akishangilia bao na wenzake.
Matokeo ya michezo mingine iliyochezwa hadi tunakwenda mitamboni ni: Aston Villa 1 - 2 Bournemouth Crystal Palace 1 - 0 Norwich Southampton 3 - 1 Newcastle Swansea City 1 - 0 Chelsea Watford 1 - 1 Everton.
Post a Comment