MANCHESTER, ENGLAND
LOUIS VAN GAAL bado yuko
kwenye mchecheto mkubwa baada ya kuwaita wachezaji wake mmoja mmoja kabla ya
kuivaa Manchester City kwenye Ligi Kuu England, Jumapili.
Mdachi huyo alifanya
kama alivyofanya baada ya kipigo kutoka kwa Midtjylland kwenye Europa League
mwezi uliopita, wakati alipowaita wachezaji wake mmoja mmoja ili kujieleza kitu
gani kimekuwa tatizo kwao.
Na sasa baada ya
kipigo kutoka kwa West Brom kwenye Ligi Kuu England na kisha kutupwa nje ya
Europa League na mahasimu wao Liverpool, Van Gaal ameona kuna shida kwenye
kikosi chake na hivyo kuwaweka kikao wachezaji wake kabla ya mchezo huo.
Kila mchezaji
aliyecheza mechi ya Liverpool aliitwa ofisini na bosi huyo Ijumaa iliyopita
kutoa maelezo akieleza sababu zinazofanya timu kufanya vibaya, ambapo kila
mmoja alitumia dakika 15 kujieleza.
Wakati huo, Van Gaal
alisema hakuna aibu yoyote kwa timu yake iliyowekeza Pauni 250 milioni kwa
kununua wachezaji kama kupitwa pointi kibao na timu kama Leicester City, ambayo
kikosi chao ni gharama ndogo sana.
baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Liverpool
"Sidhani kama
imekuwa aibu. Soka ni mchezo na wanachofanya Leicester City ni kuufanya mchezo
kuwa mzuri. Hii ina maana kwamba pesa si kila kitu,” alisema.
Kikosi hicho kiko
kwenye nafasi ya sita na kipigo katika mchezo dhidi ya Manchester City kunamfanya
kocha Van Gaal kukubali kwamba kikosi chake kitashindwa kumaliza katika nafasi
ya nne.
Man United baadaye
itafuatiwa na michezo dhidi ya Everton, Tottenham na West Ham katika mchezo wa
maruano wa Kombe la FA raundi ya sita.
Mdachi huyo anajua
kuanguka kutamfanya kumaliza utawala wake Old Trafford na anahitaji wachezaji
wake kumaliza msimu kwa mafanikio.
Van Gaal anatarajia
kurejea kwa Ashley Young kutaongeza mashambulizi zaidi wakati Ander Herrera anatajiwa
kupona haraka majeraha yake.
Post a Comment